Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo OSAMA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo OSAMA. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 7 Mei 2011

AL QAEDA IMETHIBITISHA KIFO CHA OSAMA KUPITIA MITANDAO YA KIJIHAD.

Al-Qaeda imethibitisha kifo cha kiongozi wake, Osama Bin Laden, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo na kutangazwa kupitia mitandao mbalimbali ya itikadi kali.
Taarifa
Taarifa inayothibitisha kifo.

Tarifa hiyo imesema damu ya kiongozi huyo "haitapotea" na kuwa al-Qaeda itaendelea kushambulia Marekani na washirika wake.
Kifo cha Bin Laden kitakuwa "laana" kwa Marekani, na kutoa wito kwa Pakistan kuanza harakati, imesema taarifa hiyo.
Bin Laden alipigwa risasi na kufa siku ya Jumatatu, wakati makomando wa Marekani walipovamia nyumba yake katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan.
 

Uvamizi huo ulifanywa bila ya mamlaka za Pakistan kufahamu, na hivyo kuongeza mvutano kati ya nchi hizo mbili.
Mikutano kadhaa ya hadhara ilifanyika nchini Pakistan siku ya Ijumaa, kupinga hatua hiyo.
Taarifa hiyo iliyochapishwa katika mitandao yenye itikadi kali imesema sauti ya kiongozi huyo wa al-Qaeda iliyorekodiwa wiki moja kabla ya kifo chake itatolewa hivi karibuni.
Nyumba
Makazi ya Bin Laden, Pakistan

"Damu ya Osama Bin Laden itaendelea kubaki, kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, laana inayowafuata wamarekani na jamaa zao, itawafuata ndani na nje ya nchi zao," imeonya taarifa hiyo.
"Furaha yao itakuwa masikitiko, na damu yao itachanganyika na machozi. Tunatoa wito kwa Waisilamu wenzetu nchini Pakistan, ambao katika ardhi yao Sheikh Osama aliuawa, wasimame na kupambana."
Waandishi wa habari wanasema Wapakistani wengi wamekasirishwa na kile wanachoona kama Marekani kuingilia uhuru wa nchi yao.

Pia wanaishutumu serikali ya Pakistan kwa kuruhusu makomando wa Marekani kufanya shughuli zao, ingawa maafisa wanakanusha kuwa walifahamishwa.
Karibu watu 1,000 walikusanyika katikati ya mji wa Abbotabad baada ya sala ya Ijumaa, limeripoti shirika la habari la AFP.
Walichoma moto matairi ya magari, kuweka vikwazo katika barabara kuu na kupiga kelele wakisema "Hapana Marekani" na "magaidi, magaidi, Marekani ni magaidi".
Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Rawalpindi amesema maandamano ya kupinga Marekani yalikuwa madogo kuliko yalivyotarajiwa, huku watu 50 wakijitokeza.

Ijumaa, 6 Mei 2011

OBAMA ASEMA PICHA ZA MAUAJI YA OSAMA HAZITACHAPISHWA NA KUTOLEWA HADHARANI.

Osama bin Laden
Rais Obama amesema picha za mwili wa Osama huenda zikachochea chuki
Rais Barack Obama ameamua kuwa picha za Osama Bin Laden, aliyeuwawa siku ya jumatatu, zisichapishwe.
Maafisa wa Marekani wamekuwa wakijadili iwapo wachapishe picha za mwili wa Bin Laden kukabili habari za uongo kuwa hakuuawa.
Lakini Bw Obama anaamini kuwa picha hizo huenda zikazua hisia kali akisema, '' sisi hatutaki kuonyesha picha hizi kama kikombe cha kujivunia cha kumwonyesha kila mtu."
Kiongozi huyo wa al- Qaeda alipigwa risasi katika uvamizi jumatatu iliyopita na vikozi maalum vya Marekani, Kaskazini mwa Pakistan.
Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema kuwa rais Obama ameamua wazi kuwa kutoa picha hizo hazina thamani yeyote kwani huenda ikatishia maisha ya raia.
Bw Obama amefichua uamuzi huo wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS.
Uamuzi huo ulifikiwa wakati maafisa wa Marekani walianza kuchunguza habari kwenye kompyuta, simu za rununu na vifaa vingine vya kuhifadhi habari ambavyo vilipatikana wakati wa uvamizi huo katika eneo la Abbottabad, ambapo Bin Laden alikuwa amejificha.
Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder amesema serikali hiyo inatarajia kuongeza majina mengine kwenye orodha ya magaidi wanaotakikana na Marekani, kufuatia habari walizopata katika nyumba ya Bin Laden.
Laini mbili za simu na euro 500 ($745; £450) zilipatikana zime shonelewa kwenye nguo ya Bin Laden, kana kwamba angehitajika kutoroka kwa haraka.
Wakosoaji wameelezea wasiwasi wao kuhusu uhalali wa oparesheni hiyo, baada ya Marekani kubadilisha maelezo kuhusiana na kuuwawa wa Bin Laden akiwa ajajihami kwa silaha.

Jumatano, 4 Mei 2011

KUNDI LA HAMAS LALAANI MAUAJI YA OSAMA

Wamarekani wameendelea kushangilia kuuliwa kwa Osama bin Laden huku kiongozi wa kundi la Hamas la Palestina akilaani mauaji hayo. Picha na habari zaidi za jinsi Osama bin Laden alivyouliwa zimeanza kujitokeza.
Wamarekani wameendelea kushangilia kuuliwa kwa Osama bin Laden huku kiongozi wa kundi la Hamas la Palestina akilaani mauaji hayo. Picha na habari zaidi za jinsi Osama bin Laden alivyouliwa zimeanza kujitokeza.
Osama bin Laden ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda aliuliwa kwa kupigwa risasi ya jicho la kushoto baada ya kukataa kujisalimisha kwa majeshi ya Marekani.

Rais wa Marekani, Barack Obama pamoja na maafisa wake wa ulinzi na CIA walilifuatilia shambulizi la kumuua Osama bin Laden LIVE kupitia video zilizokuwa zikirekodiwa kwa kutumia video kamera zilizowekwa kwenye helmet za makomandoo wa Marekani walioivamia nyumba ya Osama.

Picha za tukio hilo zilizotolewa na televisheni ya ABC zilionyesha damu zikiwa zimetapakaa kwenye chumba ambacho Osama bin Laden alikuwemo.

Osama aliuliwa kwa kupigwa risasi kwenye jicho lake la kushoto. Maiti yake ilichukuliwa na kupelekwa kwenye kambi ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan.

Baada ya vipimo vya DNA kuthibitisha kwa asilimia 99 kuwa mtu waliyemuua alikuwa ni Osama bin Laden baada ya kulinganishwa na vipimo vya DNA vya ndugu zake, maiti yake ilizikwa baharini baada ya Saudi Arabia na nchi zingine kuukataa mwili wake.

Helikopta moja kati ya nne za jeshi la Marekani zilizotumika kufanya mashambulizi toka angani, ilitunguliwa na roketi zilizorushwa na wapambe wa Osama bin Laden.

Nyumba aliyokuwa akiishi Osama ilikuwa takribani mita 200 toka kituo cha polisi na kilomita mbili toka kambi ya jeshi la Pakistan.

Taarifa ya Marekani ilisema kuwa maafisa wa Pakistan walikuwa hawajui kuwa Osama alikuwa amejificha kwenye jumba hilo lenye thamani ya dola milioni moja ambalo lilijengwa miaka mitano iliyopita likiwa na uzio mrefu wa kuta nene.

Wamarekani wameendelea kushangilia kuuliwa kwa Osama bin Laden ambaye alikuwa ndiye mtu aliyekuwa akitafutwa sana kuliko watu wote duniani.

Kiongozi wa Hamas katika ukanda wa Gazza, Ismail Haniyeh akiongelea kuuliwa kwa bin Laden alisema kuwa kuuliwa kwa bin Laden ni muendelezo wa umwagaji damu za Waarabu na waislamu unaofanywa na Marekani.

"Tunalaani kuuliwa kwa shujaa mtukufu wa Waarabu, Osama bin Laden na tunamuomba Mwenyezimungu amrehemu na kumweka mahali pema pamoja na waja wake wema", alisema kiongozi huyo wa Hamas.