Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MOTO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MOTO. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 30 Novemba 2011

PICHA YA LEO; VITUKO VYA PAKA, AKATAA KUONDOKA ETI KISA MOTO NA MOSHI!!!? DUKA LA MWAIBALE HALIKUUNGUA NA MOTO HUO.

 HASARA YAKADIRIWA KUWA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 10, POLENI WANATUNDUMA.

 NDIMI ZA MOTO ZIKIENDELEA KUTEKETEZA SOKO LA TUNDUMA MBEYA
 PAKA JUU YA DUKA (KULIA) AKIWA AMEGANDA HUKU MOSHI UKIA UMETANDA NA HATIMAYE DUKA HILO HALIKUGUSWA NA MOTO HUO MJINI TUNDUMA
 MOTO UKIENDELEA KUTEKETEZA SOKO LA TUNDUMA WILAYANI MBOZI MKOANI MBEYA JUZI.
Credits;kalulunga.blogspot.com

Jumatatu, 12 Septemba 2011

AJALI YA MOTO HUKO KENYA YAUA ZAIDI YA 100 BAADA YA BOMBA LA MAFUTA KULIPUKA.

Waokozi wakisaidia watu baada ya Bomba kulipuka mjini Nairobi

Zaidi ya watu mia moja wamekufa baada ya bomba la mafuta kupasuka na kulipuka katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, polisi wamesema.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la viwandani la Lunga Lunga na askari wa zima moto walipambana na moto mkali ambao ulikuwa ukitishia makazi ya watu mjini humo.
Bomba hilo la mafuta limepita katika makazi ya watu wengi kwenye mitaa ya mabanda katikati ya mji wa Nairobi na Uwanja wa ndege.
Zaidi ya majeruhi 100 wamepelekwa hospitali, maafisa wanasema.
Msemaji wa magari ya huduma za dharura alisema waathirika wengi waliungua kiasi cha kutotambulika.
Taarifa zinasema mlipuko huo huenda umesababishwa na kishungi cha sigara kilichotupwa katika mtaro wa maji ambao ulikuwa ukielea mafuta.
Mafuta hayo yalivuja kutoka kwenye tangi moja katika ghala linalomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Kenya, msemaji wa polisi Charles Owino ameliambia shirika la habari la Reuters.

‘Miili yaelea’


Polisi na jeshi wameweka vizuizi katika eneo hilo, ambapo wakazi walisema kuvuja kwa mafuta kwenye bomba hilo na kusababisha watu wengi kukimbilia kuchota mafuta yaliyovuja.
"Kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko, mlipuko mkubwa, na moshi na moto ukiwaka juu angani," mkazi mmoja Joseph Mwego aliliambia shirika la habari la AFP.
Baadhi ya majeruhi wakipelewa hospitali

Sehemu ya miili ilionekana ikiungua kiasi cha mita 300 (futi 1,000) karibu na eneo la tukio, wenyeji walisema.
Miili mingine likuwa inaelea katika mto karibu na eneo hilo ambapo watu walioungua iliripotiwa waliruka baada ya kushika moto.
Vibanda vilivyoezekwa kwa mabati vimejengwa karibu kabisa na bomba hilo, wakazi walisema.
Kumekuwa na vifo vingine ambavyo vimetokana na watu kuchota mafuta yanayovuja: Zaidi ya watu mia moja walikufa eneo la Molo, magharibi mwa Kenya mwaka 2009 baada ya lori la mafuta kupinduka na moto kulipuka

Ijumaa, 8 Julai 2011

AJALI YA MOTO MJINI NACHINGWEA JANA. DUKA LA MANGI LAUNGUA NA KUTEKETEZA MALI KADHAA, CHANZO HAKIJAJULIKANA BADO.

Wananchi wakishuhudia nyumba ya mfanyabiashara aitwae Mangi British ikiungua moto.
Moto unaanza kukolea

Baadhi ya magari mabovu yaliyokuwa jirani yakiondolewa
Mali chache ziliokolewa na wasamria wema, changamoto ni kuwa mji wa Nachingwea hauna gari la zimamoto pamoja na kuwa kuna uwanja mkubwa wa ndege hapa jirani. Inasemekana duka lililoungua ni miongoni ya maduka makubwa hapa wilayani Nachingwea.

Jumapili, 1 Mei 2011

SHERIA IMECHUKUA MKONDO WAKE, SASA HAKI IONEKANE IMETENDEKA.

MKURUGENZI wa Hoteli ya Kitalii ya South Beach Hotel ya jijini Dar es Salaam, Bw. Salim Nathoo (53), amepandishwa kizimbani juma lililopita katika Mahakama ya wilaya ya Temeke. Nathoo ambaye ni mkazi wa Mikocheni ‘A’ alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Khasim Mkwawa wa mahakama hiyo.

Mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo alitambulika kwa jina la John Mwangiombo (32).

Upande wa Mashitaka uliongozwa na Mwendesha Mashtaka, Inspekta wa Polisi Dastan Kombe na kudai kuwa, washitakiwa hao walitenda kosa hilo Aprili 10 mwaka huu majira ya saa 6.30 usiku eneo la Mjimwema Kigamboni.

Washitakiwa hao walishirikiana kwa pamoja kumpiga na kumchoma moto kijana Lila Hussen (34) na kumsababishia kifo kwa kumuhisi mwizi mara alipoingia hotelini hapo.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Kesi iliahirishwa hadi Mei 2, mwaka huu kwa kutajwa tena na washitakiwa watakwenda kujibu shtaka hilo mahakama kuu.

Awali imedaiwa kuwa marehemu Lila alichomwa moto na washtakiwa hao baada ya kuingia hotelini hapo kwa ajili ya kuwatafuta wageni wake raia wa kigeni aliowasindikiza hotelini hapo jana yake na mara alipoingia hotelini hapo kwa kuwa hakuwa na muonekano mzuri wa hadhi ya kuwa hotelini hapo mmiliki huyo alitoa agizo la kukamatwa kijana huyo kwa kudai ni mwizi na baadae walimmwagia mafuta na kumvisha tairi na kumchoma moto na alianza kuungua huku wageni wake wakiwa hawajui kinachoendelea.

Taarifa ziliwafikia jamaa zake anaofanya nao kazi maeneo ya feri na walifika hapo na kumuokoa kijana huyo na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Na muda machache baadae mkurugenzi huyo alipogundua kuwa si mwizi na kuona alifanya makosa alianza hatua za kukimbia nchini na aliwezwa kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere na kufikishwa kituo cha polisi.

Jumapili, 17 Aprili 2011

HAKI ZA BINADAMU ZIPO KWELI JAMANI?

Yule kijana wa Kigamboni aitwae Lillah ambaye juma lilopita alilipotiwa kuchomwa moto huko south beach kigamboni amefariki dunia jana na anatarajiwa kuzikwa leo huko mjimwema kigamboni. Matukio haya ya watu kujichukulia sheria mkononi nimeyazungumzia sana na tunaona madhara yake yanavyojionesha. Lillah yeye alikamatwa na walinzi wa south beach kwa tuhuma za kuzamia disco bila kuwa na tiketi, akapelekwa kwa meneja wa hoteli ambaye aliamuru achomwe moto na amri ikatekelezwa kwa kumwagiwa petroli na kupigwa kiberiti, alikimbilia baharini na baadae wasamalia walimpeleka hospitali kigamboni akaamishiwa muhimbili, amefariki jana,ameacha mke na watoto. Meneja na walinzi wawili  walikamatwa, sijui kama waliachiwa, TUNAOMBA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE NA HAKI IONEKANE KUWA IMETENDEKA. Buriani Lillah.