Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo GLOBALPUBLISHERS. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo GLOBALPUBLISHERS. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 14 Agosti 2013

JERAHA LA SHEIKH PONDA LIMESABABISHWANA NINI? MADAKTARI WA MOI WANASEMA HAWAJUI SABABU PONDA ALIKUJA PALE AKIWA AMESHONWA ALIKOTOKA, MAANA YAKE PONDA ASEME WALIOMSHONA MWANZO WALIONA NINI AU HAO MADAKTARI WAJITOKEZE KUTUTEGULIA KITENDAWILI HIKI.

NI VIGUMU KUJUA JERAHA LA SHEIKH PONDA LILISABABISHWA NA KITU GANI - MOI

 
Sheikh Ponda (54) akiwa katika chumba maalum katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
 

TAARIFA KUHUSU MAJERAHA YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA KUTOKA MOI
Sheikh Ponda Issa Ponda (54) alipokelewa hapa taasisi ya tiba ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI jana tarehe 11/8/2013 saa 7.30 jioni akitokea hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupokelewa alionekana akiwa na majeraha chini ya bega la mkono wa kulia lililokuwa limeshonwa mbele na nyuma madaktari wetu walifanya uchunguzi na kushauri afanyiwe kipimo cha X-ray ili kubaini kama kuna mvunjiko kwenye sehemu ya jeraha tathimini ya madaktari baada ya kupata majibu ya X-ray ilionyesha alikuwa na mvunjiko bila mifupa kupishana vivyo hivyo kidonda hakikuwa katika hali nzuri licha ya tiba ya mwanzo na iliamuliwa afanyiwe upasuaji mpya ili kuzuia maambukizi kama kingeachwa hivyo.
    
    KWA HIYO
    1- kufuatana na tiba ya awali aliyopata ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha kabla ya kufikishwa MOI imekuwa vigumu kujua kama jeraha lilisababishwa na kitu gani
    2- kipimo cha X-ray kilionyesha kwamba alikuwa amepata mvunjiko wa mfupa mkubwa wa bega bila mifupa kupishana
    3- hivyo basi Sheikh Ponda Issa Ponda anaendelea na matibabu baada ya upasuaji.
Imetolewa na :
    Mkurugenzi Mtendaji
    Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu MOI
     Agosti 12, 2013
Credits;Globalpublishers

Ijumaa, 7 Desemba 2012

DAKTARI WA ‘MOI’ MUHIMBILI, NESI WAKE MBARONI KWA RUSHWA, WAPANDISHWA KIZIMBANI KISUTU JANA.


Daktari Matiko (katikati) akiongozwa na Afisa wa Takukuru (nyuma yake).  Aliyetangulia ni wakili anayemtetea, Paschal Kamala
 
…Akielekea kizimbani kwa upole.
 
Nesi Kimwomwe (kulia) naye akielekea kizimbani kusomewa mashitaka yake.


Uchungu wa safari ya kuelekea kizimbani.
                    Ndugu na jamaa wakifuata nyuma kwa ajili ya kusikiliza kesi za wapendwa wao.

Jumatano, 5 Desemba 2012

TAMTHILIYA YA ‘SIRI YA MTUNGI’ KUONYESHWA KWENYE LUNINGA NCHINI, INAELEZEA MAPENZI YA USALITI NA USHIRIKINA.

  
Mkurugenzi wa MFDI, John Riber, akiongea na waliohudhuria uzinduzi huo (hawapo pichani).
  Mhusika mkuu wa tamthiliya hiyo aliyetumia jina la Cheche.
  
   Wadau wakishuhudia uzinduzi huo.
  Wadau wakiifuatilia kwa makini hafla hiyo.
  Hawa ni miongoni mwa  wasanii 600 walioshiriki tamthiliya hiyo.
 
  Monalisa ambaye ni miongoni mwa mastaa wa filamu nchini walioshiriki kwenye tamthiliya hiyo.
TAMTHILIYA  mpya itwayo Siri ya Mtungi kutoka kampuni ya watu wa Marekani ya Media For Development Internalional (MFDI)  inatarajiwa kuanza kuonekana kwenye vituo vya runinga vya ITV na EATV baada ya siku ya uhuru 9 Desemba 2012. Tamthiliya hiyo imezinduliwa leo katika ofisi za MFDI zilizopo Msasani Jijini Dar es Salaam ikiwa inahusu penzi lililoletwa na woga, ushirikina, na usaliti, ucheshi na mengineyo.
     (PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

Alhamisi, 22 Novemba 2012

WALIOMUUA SWETU FUNDIKIRA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA.

.....ndugu wakilia

...ilikuwa ni saa ya majonzi na huzuni
Watuhumiwa wakiwa mahakamani kabla ya hukumu kusomwa. kutoka kulia ni Rhoda Robert, Ally Gube na Mohamed Ally.
safari ya huzuni ya Rhoda Robert kuanza maisha mapya gerezani mara baada ya hukumu...
Leo ilikuwa ndiyo siku ya hukumu dhidi ya watuhumiwa watatu wa mauaji ya marehemu Swetu Fundikira aliyeuawa kwa kupigwa miaka miwili iliyopita. Mara baada ya watuhumiwa hao kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa, ndugu na jamaa wa marehemu waliangua kilio na wengine hadi kuzimia kama walivyoshuhudiwa na paparazi wetu aliyeweka kambi mahakamani hapo.

PICHA: ISSA MNALLY/GPL

Jumatatu, 15 Oktoba 2012

MTUHUMIWA WA USAFIRISHAJI MADAWA YA KULEVYA AACHIWA HURU, NI ALHAJI MINTANGA.


Alhaji Shaaban Mintanga akiwa chini ya ulinzi mkali wakati wa kesi yake.
Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Alhaji Shaaban Mintanga, leo ameachiwa huru baada ya kushinda kesi yake ya kukamtwa na madawa ya kulevya. Mintanga ameachiwa huru baada ya kusota rumande tangu April 4 mwaka 2008.

Jumanne, 11 Septemba 2012

SIMBA YANYAKUA NGAO YA JAMII KWA KUIFUNGA AZAM GOLI 3-2.

SIMBA YAIGONGA AZAM 3-2, YATWAA NGAO YA JAMII

 

Mshambuliaji wa Simba SC, Mghana Daniel Akuffo akijiandaa kupiga penati wakati wa mpambano wao wa Ngao ya Jamii leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar

HABARI TOKA TFF-KELVIN YONDAN NA MBUYI TWITE NI WACHEZAJI HALALI WA YANGA.

Ramadhan Chombo ‘Redondo’
------
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 11, 2012
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba 10 mwaka huu) ili kupitia na kutoa uamuzi/ushauri kwa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa mbele yake.
Wajumbe sita kati ya saba waliopo walihudhuria kikao hicho chini ya Mwenyekiti Alex Mgongolwa. Wajumbe hao ni Hussein Mwamba, Imani Madega, Ismail Aden Rage, Llyod Nchunga na Omari Gumbo.
Suala la ugombea wa Michael Wambura katika FAM
Michael Wambura aliomba uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) katika uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana. Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliondoa jina lake kwa kukosa sifa ya kugombea nafasi hiyo.
Wambura hakuridhika na uamuzi huo akapeleka shauri lake Kamati ya Nidhamu ya TFF. Kamati hiyo katika uamuzi wake ilisema haina mamlaka ya kushughulikia shauri hilo. Baadaye Wambura alikata rufani katika Kamati ya Rufani ya TFF ambayo ilimpa haki ya kugombea.
Kutokana na mkanganyiko huo wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwa na uamuzi wa mwisho katika masuala ya uchaguzi ya wanachama wa TFF, na uamuzi wa Kamati ya Rufani kuhusu uchaguzi wa mwanachama wa TFF, Sekretarieti ya TFF iliomba mwongozo wa kisheria kwa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji.
Kwa vile Kamati hizo mbili (Uchaguzi na Rufani) haziko katika mtiririko wa moja kwa moja wa utoaji maamuzi, Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliishauri Sekretarieti ya TFF kuliandikia Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ili kupata muongozo juu ya suala hilo.
Katika muongozo wake, FIFA ilitoa maoni kuwa kwa mujibu wa Katiba ya TFF chombo cha mwisho cha rufani katika masuala ya uchaguzi kwa wanachama wa TFF ni Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Hata hivyo, FIFA ilishauri kuwa si vizuri chombo kimoja kikawa msimamizi wa uchaguzi, na chenyewe tena ndiyo kiwe cha mwisho katika uamuzi kwenye uchaguzi husika.
Hivyo, Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji imetoa mapendekezo mawili kwenda Kamati ya Utendaji kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ili kiwepo chombo kingine cha rufani pale mgombea anapopinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Mapendekezo hayo ni; Iundwe Kamati ambayo itakuwa inasikiliza rufani zote zinazotokana na uamuzi uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF isiwe chombo cha mwisho cha uamuzi kwa rufani zinazotokana na uchaguzi wa wanachama wa TFF.
 
AU. Rufani zote zinazotokana na uchaguzi wa wanachama wa TFF zisikilizwe na Kamati ya Rufani ya TFF. Kwa maana hiyo Kamati ya Rufani ya TFF ndiyo kiwe chombo cha mwisho kwa wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwasilisha malalamiko yao.
 
USAJILI/PINGAMIZI DHIDI YA WACHEZAJI
Musa Hassan Mgosi, Ayoub Hassan Isiko
Mchezaji Musa Hassan Mgosi ameombewa usajili Ruvu JKT kutoka DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), na Ayoub Hassan Isiko ameombewa usajili Mtibwa Sugar kutoka Bull FC ya Uganda. Wachezaji hao hawaruhusiwi kuchezea timu hizo mpaka Hati zao za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) zitakapokuwa zimepatikana.
Toto dhidi ya Kagera Sugar kumsaini Enyinna Darlinton Ariwodo
Toto Africans ilipinga usajili wa Enyinna Darlinton kwa timu ya Kagera Sugar kwa vile bado ina mkataba wa mchezaji huyo ambao unamalizika mwakani.
Kwa upande wake Kagera Sugar ilisema imemsaini mchezaji huyo kwa vile Toto Africans imeshindwa kumlipa mshahara ambapo kuna makubaliano rasmi kati ya Ariwodo kuwa klabu hiyo ikishindwa kumlipa mshahara anaruhusiwa kuondoka.
Uamuzi wa Kamati ni kuwa Ariwodo ni mchezaji halali wa Kagera Sugar kwa vile Toto Africans ilishindwa kutimiza masharti ya mkataba.
 
Ramadhan Chombo ‘Redondo’
Redondo ameidhinishwa kuchezea Simba kwa kuzingatia mchezo wa haki na uungwana (Fair Play) baada ya klabu hiyo na ile ya Azam kufikia makubaliano kuhusu mchezaji huyo.
Mchezaji David Luhende kusajiliwa Yanga
Yanga ilikiri kutolipa ada ya uhamisho ya sh. milioni 5 kama walivyokubaliana na Kagera Sugar. Awali waliipa Kagera Sugar hundi iliyogonga mwamba benki (bounced cheque). Shauri hilo lilimalizwa kwa Yanga imetakiwa kulipa fedha hizo ndani ya siku 21 kuanzia Septemba 10 mwaka huu.
 
Super Falcon dhidi ya Edward Christopher kusaini Simba
Simba imepewa siku 21 kuanzia Septemba 10 mwaka huu iwe imeilipa Super Falcon fedha za matunzo (compensation) kwa vile ndiyo iliyomlea mchezaji Edward Christopher aliyesajiliwa katika klabu hiyo.
 
Toto Africans dhidi ya Mohamed Soud kusajiliwa Coastal Union
Toto Africans iliweka pingamizi kwa maelezo kuwa bado ina mkataba na mchezaji huyo. Hivyo kwa msingi wa Fair Play, mchezaji huyo ameidhinishwa Coastal Union baada ya makubaliono kati ya klabu.
 
Rollingstone dhidi ya Kigi Makassy kusajiliwa Simba
Simba imetakiwa kuilipa Rollingstone gharama za matunzo ilizoingia wakati ikiwa na mchezaji huyo kwa kuzingatia kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
 
Super Falcon dhidi ya Sultan Juma Shija kusajiliwa Coastal Union
Uamuzi wa Kamati ni kuwa Shija atachezea Coastal Union, na kwa vile yuko chini ya umri wa miaka 23, Coastal Union itailipa Super Falcon fidia ya fedha ilizotumia kumhudumia mchezaji huyo.
 
African Lyon dhidi ya Razak Khalfan kusaini Coastal
Lyon imesema bado ina mkataba na mchezaji huyo. Kamati imebaini kuwa mkataba wa mchezaji huyo na Lyon umemalizika, hivyo ni mchezaji halali wa Coastal Union.
 
Flamingo dhidi ya Kelvin Friday kusajiliwa Azam
Friday ruksa kucheza Azam, lakini klabu hiyo imepewa siku 21 kuanzia Septemba 10 mwaka huu kuilipa Flamingo gharama za kuvunja mkataba.
 
Super Falcon dhidi ya Robert Joseph Mkhotya kusaini African Lyon
Lyon imeagizwa kuilipa Super Falcon sh. milioni moja ikiwa ni fidia ya kuvunja mkataba wa mchezaji huyo ambaye imemsajili. Fedha hizo zitalipwa kwa awamu nne kutokana na makato ya mlango yatakayofanywa na TFF. Falcon itapokea malipo hayo kupitia TFF.
 
Oljoro JKT dhidi ya Othman Hassan kusajiliwa Coastal
Kwa mujibu wa rekodi za TFF, mkataba wa mchezaji huyo na Oljoro JKT unamalizika mwakani. Hivyo, Othman Hassan ni mchezaji halali wa Oljoro JKT kwa vile bado ana mkataba na klabu hiyo.
 
Yanga dhidi ya Simba kuacha wachezaji wanne
Kamati imetupa pingamizi hizo kwa vile hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wachezaji juu ya kuvunjiwa mikataba yao. Wachezaji hao walioachwa na Simba ni Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiavanga na Lino Masombo.
Ikiwa wachezaji hao watakuwa na malalamiko kuhusu kuvunjiwa mikataba suala hilo litafikishwa katika Kamati kwa ajili ya kusikilizwa na kutolewa uamuzi.
 
Mbuyu Twite
Kwa mujibu wa Ibara ya 18(3) ya Kanuni za Hadhi na Uhamisho wa Wachezaji wa Kimataifa za FIFA, Yanga ilifuata taratibu zote katika kumsajili Mbuyu Twite, hivyo ni mchezaji wake halali. Hata hivyo, kwa vile Yanga imekiri kuwa mchezaji huyo alichukua dola 32,000 za Simba na kukiri kuzirejesha, kwa msingi wa kanuni ya Fair Play, Kamati imeipa Yanga siku 21 iwe imelipa fedha hizo Simba.
 
Kelvin Yondani
Kwa mujibu wa Ibara ya 44(3) ya Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za TFF, Yanga ilifuata taratibu zote katika kumsajili Kelvin Yondani, hivyo ni mchezaji wake halali.
Kwa vile Simba imesema mchezaji huyo vilevile alisaini mkataba na klabu yao, imetakiwa kupitia mamlaka nyingine kuthibitisha hilo, na baada ya uthibitisho iwasilishe malalamiko yake kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, au mamlaka zozote za kisheria kwa mujibu wa madai/lalamiko husika.
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji.

Jumanne, 21 Agosti 2012

MKOMBOZI WA TANZANIA TOKA MAKUCHA YA RUSHWA NI MTANZANIA MWENYEWE.

Nani ataikomboa Tanzania kwenye makucha ya rushwa?

Jenerali Ulimwengu.
HATA kwenye maandiko ya vitabu vitakatifu tunaambiwa kuwa, Mwenyezi Mungu baada ya uumbaji wa dunia alimweka Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni na kuwapa uhuru wa kula matunda yote katika  bustani ile isipokuwa matunda ya mti uliokuwepo katikati ya bustani.
Kwa wanaofuatilia maandiko ya dini wanafahamu kilichotokea. Hapa nchini kuna sheria na maneno mengi yanayowataka viongozi na raia wa kawaida kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
Lakini ajabu ni kwamba hivi majuzi tumesikia shutuma nzito za vitendo vya rushwa zikitolewa ndani ya Bunge vikiwahusisha viongozi wa Kamati za Bunge hususan Kamati ya Nishati na Madini, Hesabu za Serikali za Mitaa na Hesabu ya Mashirika ya Umma.
Kiukweli  tunachokiona si cha ajabu, maana ni taswira ya mambo ambayo sisi kama jamii tumeyakubali, tumeyapokea na kuyafanya kuwa sehemu ya maisha yetu. Limekuwa ni jambo la kawaida mtumishi fulani kula rushwa na kujitajirisha harakaharaka na watu kumsifu kwamba eti ana akili sana!
Katika baadhi ya vitengo kama vile mahakamani, polisi, idara za ardhi au maliasili kama ambavyo iliwahi kuaninishwa na Tume ya Joseph Warioba, ulaji wa mlungula ni  tabia ambayo baada ya muda imegeuka na kuwa ‘mazoea’ na hatimaye kuwa haki.
Wanaofanya hivyo wanajiona wana haki ya kupewa rushwa, mahakamani mafaili yanafichwa na hata polisi, sehemu ambazo zilipaswa kuwa mstari wa mbele kutetea haki ya mtu.
Kila mtu pale alipo aiangalie jamii yetu na matendo yake nyakati hizi, naweza kusema kuwa tunaishi katika jamii ya watu wanaopenda rushwa, maana hata bei za bidhaa zipande kiasi gani hakuna mtu anayethubutu kusema kwa sauti kuwa tunalanguliwa!
Kwa kweli inasikitisha  zaidi kwa namna Watanzania na serikali yao wanavyoonekana kwa taswira ya rushwa. Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika uhai wake na uongozi wake alikemea kwa vitendo rushwa na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kupunguza vitendo vya rushwa nchini.
 Kwa msimamo huo huduma za jamii kama vile elimu ilikidhi haja kwani wanafunzi walikuwa wakifundishwa na kugawiwa madaftari na hata kalamu bure, afya- watu walikuwa wakitibiwa bure na dawa zilikuwa zikipatikana, barabara- zilijengwa japokuwa kasi haikuwa kubwa, maji safi na salama yaliwafikia wananchi wengi vijijini bila mizengwe yoyote.
Sifa ya nchi ya Tanzania hakika ilikuwa nzuri machoni mwa wananchi na nje ya nchi. Ilikuwa ni vigumu kuona kiongozi wa serikali au shirika la umma akijenga hekalu ambalo halilingani na mshahara au kipato chake.
Leo hii kiongozi anaweza kusema kwenye bajeti ya serikali kuwa jengo fulani la serikali halitajengwa kwa kuwa bajeti haitoshi lakini huyohuyo akanunua magari yake mawili ya kifahari na kujenga nyumba mbili au tatu. Utajiuliza fedha amepata wapi? Jibu ni rahisi, ni rushwa tu.
Bahati mbaya baada ya uongozi wa Mwalimu, dhambi ya rushwa ikaanza taratibu kutambaa ndani ya jamii na sasa imekuwa kubwa mithili ya kansa isiyotibika. Tunashuhudia rushwa waziwazi katika chaguzi ambapo hata baadhi ya wana habari wanatajwa kujihusisha na rushwa. Hii ni mbaya sana. Wakati mwingine uhitaji hata ushahidi, maana maandishi yao na vitendo vyao vinajionesha.
Nimpongeze mwanahabari mkongwe, Jenerali Twaha  Ulimwengu ambaye amewataka wanahabari na wananchi wa Tanzania, hususan wale wanaokerwa na vitendo vya rushwa kukusanya hasira na kukemea kwa nguvu vitendo vya rushwa nchini, namuunga mkono mia kwa mia.
Alisema kuwa, kimsingi huwezi kupigana na mtu au nchi kama huna hasira, vivyohivyo inatupasa kuwa na hasira ya kutosha kupambana na adui huyu aitwaye rushwa ambaye kwa hakika amesababisha mabilioni ya shilingi za walipa kodi kupotea na kuingia katika mifuko ya watu binafsi wasio na huruma na wenzao.
Niseme bila kumung’unya maneno kwamba kama rushwa itaachiwa isambae bila kupigwa vita kwa nguvu, itamaliza taifa, tutateketea.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli

Credits; www.globalpublisherstz.info

Jumapili, 12 Agosti 2012

JOHN EVANS ATTA MILLS AMEZIKWA KWA HESHIMA JUZI HUKO GHANA.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI.


Shughuli mbalimbali za  mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra jana Agosti 10, 2012

Ijumaa, 3 Agosti 2012

MRISHO NGASSA AMEPOKELEWA KWA KISHINDO LEO HUKO MTAA WA MSIMBAZI.

Mrisho Ngassa akikabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kwa wanachama wa Simba SC.
Ngassa akionyesha jezi aliyokabidhiwa na Simba SC.
...Akiwa katika pozi na wanachama wa Simba.…


Mrisho Ngassa akikabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kwa wanachama wa Simba SC.

Ngassa akionyesha jezi aliyokabidhiwa na Simba SC.
...Akiwa katika pozi na wanachama wa Simba.
Mashabiki wa Simba waliofika kumkaribisha Ngassa wakiwa na bango la kuwakejeli watani wao,mwenye bango ni shabiki maarufu wa Simba SC Hamis Kapopo wa Songea.

Mashabiki wakimshangilia Ngassa anayeingia kwenye gari.

...Wakilisonga gari lake.

Mashabiki wakimsindikiza Ngassa wakati akiondoka Makao Makuu ya Simba.
MCHEZAJI mpya wa Simba, Mrisho Ngassa, leo amekabidhiwa jezi namba 16 atakayokuwa akiitumia kwenye klabu yake msimu huu.
Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
Kaburu alisema Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo mmoja na kwamba wapenzi wote wa Wekundu wa Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.
"Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu. Tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza muda wa mkopo wake kutoka Azam na ni imani yetu kwamba ujio wa Ngassa utaimarisha zaidi timu kwani yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, anawapenda," alisema. 
Akizungumza katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi kusajiliwa na Simba kwani ni sawa na historia kujirudia, akikumbusha kwamba baba yake mzazi, Khalfan Ngassa, aliwahi kuwa mchezaji wa klabu katika miaka ya 1990.
Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba katika ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam ambako Simba inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre Richard na James Kisaka.

(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)

KIKWETE ATIMIZA HAHDI YA KUWAFIDIA NG'OMBE WANANCHI WA MONDULI WALIOPOTEZA MIFUGO YAO KWA UKAME

MH. KIKWETE AMEGAWA NG'OMBE KWA WANANCHI MONDULI LEO, ATAFANYA HIVYO KILA MWEZI KWA WILAYA TATU.


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipowasili katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kwa ajili ya kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.…

Ijumaa, 27 Julai 2012

AZAM FC NA YANGA KUKUMBANA KIPUTE CHA FAINALI KAGAME CUP JUMAMOSI HII.

YANGA SC YAILAZA APR, YATINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME


Kikosi cha Yanga kilichoanza mechi ya leo.
TIMU ya Yanga SC imefanikiwa kuingia Fainali ya Michuano ya Kombe la Kagame leo baada ya kuilaza timu ya APR ya Rwanda bao 1-0 kwenye mchezo wa Nusu Fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Bao la Yanga limefungwa na mchezaji Hamis Kiiza katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika 0-0. Kwa matokeo haya, Yanga itakutana na Azam FC katika fainali itayochezwa Jumamosi Julai 28, 2012 katika Uwanja wa Taifa.

Jumatatu, 11 Juni 2012

ETI DIAMOND PLATNUM KAJIUNGA FREEMASONRY!!!!?


Diamond akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason.
Stori: Shakoor Jongo na Erick Evarist
SIRI imefichukua kuwa madai kwamba ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ ni memba wa jamii ya siri inayodaiwa kumwabudu shetani, Freemason a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo lakini sasa zimeshika kasi baada ya kunaswa kwa picha inayomuonesha akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason, Ijumaa Wikienda linaibumburua.
Kwa mujibu picha hiyo, tukio hilo lilijiri nchini Uingereza, mwaka jana, Diamond alipokwenda huko kwa ajili ya shoo.

MAVAZI
Ilidaiwa pia kuwa mavazi ya Diamond (meusi) yalishabihiana sawia na yale ya mtasha huyo yanayoelezwa kuwa sehemu ya mavazi ya jamii ya Freemason.

ISHARA
Kingine kilichoibua maswali ni ishara ya salamu ya wawili hao ambayo ilitengeneza nembo ya Freemason ya ‘V’ au bikari kwa namna walivyogusana kwa vidole.
Kwa mujibu wa wadau walioiona picha hiyo iliyonaswa kwenye mtandao wa Twitter, Diamond amekuwa na ishara nyingine nyingi za aina hiyo hivyo kuzidi kuzua utata kama ni memba wa jamii hiyo.
“Lakini inawezekana kwa sababu nasikia ukishajiunga unapata mafanikio ya ghafla. ‘So’ kuhusu hili, sina upande wa kusimamia,” ilisomeka sehemu ya maoni kwenye mtandao huo baada ya kuibuka mjadala mzito juu ya ishu hiyo inayozidi kushika kasi mithili ya moto wa kifuu.
“Tungeshukuru kama Diamond mwenyewe angejitokeza aseme ukweli kwani akinyamaza anazidi kutuweka njia panda,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni hayo huku ikiungwa mkono na wengi.

UNATAKA KUMSIKIA DIAMOND? SOMA HAPA
Ili kumaliza utata wa je, Diamond ni Freemason au la, Ijumaa Wikienda lilibeba jukumu la kumtafuta ili aanike ukweli wake ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Unajua mwanzoni nilikuwa sikumbuki ni lini na wapi nilipiga picha ya dizaini hiyo. ‘Anyway’, isiwe kesi, nakumbuka ilikuwa Uingereza kipindi kile nilikuwa na shoo nchini humo.
“Nakumbuka walinifuata watasha wengi tofauti lakini huyo mmoja alining’ang’ania sana nipige naye picha.
“Kwa kweli alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa lakini baadaye nikaona isiwe ishu nikampa ushirikiano alioutaka.
“Mimi sikuona matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa sababu nilikuwa sijui chochote kuhusu Freemason. Nimeijua baada ya mambo haya kuyasikia kwa sana hivi karibuni.
“Kwa hiyo inawezekana siku hiyo waliniunganisha bila mimi kujua (kicheko).”

SASA UKWELI NI UPI?
Mara kadhaa Diamond amekuwa akihusishwa na Freemason kutokana na mafanikio ya ghafla aliyoyapata na mvuto alionao kwa mashabiki wake ndani na nje ya Bongo.
Ijumaa Wikienda lilipotaka kupata ukweli kutoka kwake, Diamond alifunguka:
“Si kweli bwana, mimi nazisikia tu hizi habari kama wengine. Nasikia tu ipo hapa Bongo na kiongozi wake ni Sir Andy Chande, zaidi ya hapo sijui chochote.
“Mimi ni mtu wa swala tano na mafanikio yangu naamini Mungu ndiyo kila kitu.”

KUNA MSANII MWINGINE
Mbali na mwigizaji Jacqueline Wolper na marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ ambao wamekuwa wakitajwatajwa na mambo ya Ufreemason, Ijumaa Wikienda limetajiwa msanii mwingine ambaye yupo mbioni kujiunga akidai anakwenda kufuata utajiri.

AANZA KUPATA MAFANIKIO
Msanii huyo ambaye ni mwigizaji mwenye jina (tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuanza kupata mafanikio ya ghafla hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni na litakapomuweka kati litamrusha hewani.

Jumanne, 29 Mei 2012

AJINYONGA KWA MADAI YA UGUMU WA MAISHA


Jamaa akiwa ananing’inia muda mchache baada ya kujinyonga.
Marehemu akionekana kwa nyuma.
Mke wa marehemu akilia kwa uchungu.
Baada ya kuteremshwa chini na Wasamaria wema.
Majirani waliokusanyika eneo la tukio.
----
MWANAMME mmoja ambaye hakutambulika jina lake, aliyekuwa mkazi wa Kigogo-Mbuyuni jijini Dar es Salaam asubuhi ya kuamkia leo (Mei 29), amejinyonga kwa madai ya ugumu wa maisha uliosababishwa na kukosa ajira.
Wakizungumza na mtandao wa huu, baadhi ya majirani ambao walihojiwa walisema kuwa jamaa huyo kwa muda mrefu alikuwa hana kazi hivyo kumsababishia ugumu wa maisha ambao ulikuja kumfanya ajinyonge.
“Siku zote mwanaume ameumbwa kutafuta riziki na si kukaa kusubiri kuletewa riziki. Jamaa huyu alikuwa akikaa tu nyumbani akimuachia mkewe aende akatafute riziki, matokeo yake ndio haya,” alisema jirani mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.
Credits (Picha/ Habari: Shakoor Jongo /GPL)

Jumapili, 20 Mei 2012

SERENGETI KUDHAMINI TUZO ZA MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2011

 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda.
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti imetangaza kudhamini tuzo za Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2011 kwa sh. Milioni 150, tuzo ambazo zinaandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Udhamini huo ulitangazwa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye klabu ya City Sports Lounge, Dar es Salaam, ambapo aliambatana na viongozi wa TASWA.

Alisema kampuni yake inaona fahari kuendelea kudhamini tuzo za TASWA ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo, hivyo mwaka huu wameongeza udhamini zaidi ili…

 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda.
....... kuziboresha.
Alisema tuzo hizo zitafanyika Juni 14 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee (VIP) Dar es Salaam na kwamba wana matumaini makubwa zitakuwa bora kuliko zilizopita.
Naye Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto aliwashukuru Serengeti na kusema udhamini huo ni ishara ya namna kampuni hiyo inavyothamini wanamichezo hapa nchini na kwamba umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka sh. Milioni 80 za mwaka jana.
Hata hivyo Pinto alisema milango ipo wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza kama wadhamini washiriki kwa
vile bajeti ya tuzo hizo ambayo awali chama chake kimepanga ni sh. milioni 370, lakini hata udhamini huo unatosha kufanya kitu kizuri zaidi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando alisema Kamati Maalum ya Tuzo hizo inaendelea na mchakato wake wa kupata wanamichezo hao na kwamba kadri watakavyokuwa wanapiga hatua watatoa taarifa kwa wanahabari.
Kwa miaka mitano iliyopita walioshinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa TASWA walikuwa ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle (2007), Mary Naali (2008), ambao wote ni wanariadha, wakati 2009 na 2010 alikuwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan.

Jumatatu, 9 Aprili 2012

NDEGE YA ATC YAPATA AJALI MAPEMA LEO WAKATI IKIJARIBU KUPAA HUKO KIGOMA, ABIRIA WOTE WAMEPONA.


Ndege ya shirika la ATC muda mfupi baada ya kupata ajali mapema leo mjini Kigoma.
Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wakitoka baada ya ajali.…