Jumatano, 7 Novemba 2012

BARACK OBAMA ASHINDA TENA URAIS WA MAREKANI KWA TABU SANA.

Obama ashinda urais Marekani, Romney akubali matokeo, ampongeza

Rais Obama akiwa na familia yake kabla ya kuwahutubia wamarekani baada ya ushindi.
Rais Obama akiwa na familia yake kabla ya kuwahutubia wamarekani baada ya ushindi.
AFP

Na Sabina Chrispine Nabigambo

Rais wa Marekani Barack Obama amewashukuru wamarekani kwa kuonesha imani juu ya uongozi wake na kumpa ridhaa ya kuongoza tena taifa hilo kwa muhula wa miaka minne ijayo.

Katika hotuba yake baada ya kutangazwa kushinda rais Obama amesema kuwa kwa sasa anarejea ikulu akiwa na malengo thabiti na mwenye ari zaidi ya awali kwa lengo la kuwatumikia raia wa taifa hilo.
Obama amesema kuwa haijalishi tofauti zozote zilizopo kwa wamarekani bado kwa pamoja inawezekana kulifikisha taifa hilo mbele zaidi katika suala la maendeleo na usalama, ili kuhakikisha ndoto za wamarekani wote zinatimia.
Aidha rais Obama amemshukuru mpinzani wake Mitt Romney kwa kampeni zenye ushindani na kwamba ataendeleza ushirikiano na gavana huyo ili kuliwezesha taifa hilo kusonga mbele kwa manufaa ya wamarekani wote.
Rais Obama amemshinda mpinzani wake Mitt Romney kwa wingi wa kura za majimbo ambapo amepata jumla ya kura 303 dhidi ya kura 206 alizopata Romney,ambaye hata hivyo ameshinda Obama kwa kura za wananchi kwa asilimia 50 ya kura huku Obama akiambulia asilimia 49.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni