Cameroon yabanduliwa nje
Cameroon leo imebanduliwa nje ya fainali za kuwania kombe la mataifa huru barani Afrika zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini, licha ya kushinda mechi yao ya raundi ya pili kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Cape Verde hii leo mjini Yaunde.
Cape Verde iliilaza Cameroon kwa mabao mawili kwa bila katika mechi yao ya raundi ya kwanza.Cape Verde ambayo imeorodheshwa nyuma ya Cameroon katika orodha ya timu bora ulimwenguni, imeandikisha historia kwa kufuzu kwa fainali hizo za kuwania kombe la mataifa huru barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuishinda Indomitable Lions kwa jumla la magoli matatu kwa mawili.
Katika mechi nyingine ya kufuzu, Ethiopia ilivaana na Sudan ambapo Ethiopia imeibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila.
Katika mechi ya raundi ya kwanza Sudan ilishinda kwa mabao matano kwa matatu.
Ethiopia sasa imefuzu kupitia sheria ya goli la ugenini baada ya timu hizo kufungana jumla ya magoli matano kwa matano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni