Jumapili, 9 Septemba 2012

KIKAO CHA MGOGORO WA MPAKA WA MALAWI NA TANZANIA CHA KESHO HUENDA KIKAAHIRISHWA.


Malawi yaiomba Tanzania kuahirisha mkutano wa mpaka

Customs Office ya Kasumulu Kyela ambao ni mpaka kati ya Malawi na Tanzania.

SERIKALI ya Malawi imeomba kuahirishwa kwa mkutano wa wajumbe wanaoshiriki katika kutafuta muafaka wa mgogoro wa mpaka uliotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kesho uahirishwe.

Katika ombi hilo, ilieleza kwamba sababu kubwa ni kwamba hatua ya awali ya kuwakutanisha Wanasheria Wakuu wa nchi hizo mbili kubadilishana nyaraka muhimu ambazo Serikali zitazitumia katika kutafuta suluhu hiyo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Quent Kalichero alisema jana kwamba wakati wa mkutano wa wajumbe hao uliofanyika Lilongwe, Malawi wiki mbili zilizopita walikubaliana kwamba Wanasheria Wakuu wan chi zote mbili wanatakiwa kukaa pamoja na kubadilishana uelewa wa kisheria wa mkataba wa Anglo Germany wa mwaka 1890, hasa ibara ya 1(ii) na sehemu ya (iv) ya mkataba wa Heligoland.

Alisema mkataba wa Anglo Germany wa mwaka 1890 yalitiwa saini na Uingereza na Ujerumani ambao walikuwa wakoloni wa nchi hizo mbili wakionyesha kwamba mpaka upo katika kingo za ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania, lakini hili limepuuzwa.

Katika mahojiano yake Alhamisi wiki hii, Kalichero alisema Wizara yake imeandika barua maalum kwa wenzao wa Tanzania wakiwataka waahirishe mkutano huo kwa kuwa Wanasheria hao wakuu wa nchi hizo hawajatimiza wajibu wao kwa wakati

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni