Katiba ya JMT inaruhusu uhuru wa kutoa mawazo lakini uhuru huu usiingilie uhuru wa mwingine.
Huyu ndiye Kiongozi wa Kundi linaloitwa UAMSHO la Zanzibar ambalo ni la shughuli za mihadhara ya Kidini hasa ya Kiislam. Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya vurugu huko Zanzibar na habari zilizoenea ni kuwa Kundi hili linahusika na vurugu hizo, je ni kweli malengo ya kundi hili ni vurugu au kuna propaganda ndani yake ya kulichafua hadhi yake ili lionekane halifai!!!? Nawaasa Viongozi wa Serikali na Vyombo vya Dola kutotoa majibu ya harakaharaka juu ya vurugu za Zanzibar badala yake ifanye uchunguzi wa kina juu ya matatizo yaliyopo ili yatatuliwe. |
Mkuu acha ku0ng0pa na kuzusha mamb0 us0yafaham,uwe na ushahid km hiIi kundi Ia uamsh0 nd0 IiI0husika na uch0maji wa makanisa na menginey0!kisha nd0 unene hay0!me najua umepata uzushi wa hay0 magazeti uI0yas0ma iIa ukweIi wa hiIi swaIa huIijui kwa hy0 fwatiIia kwanza kisha nd0 uzushe manen0!ucjenge chuki dhidi ya watu ktk jamii!
JibuFutaAmar Bawaazir! yale yalikuwa mawazo yangu tu hasa kutokana na habari tunazozipata kwenye vyombo vyetu, Nakubaliana na wewe kuwa nimefanya haraka kuhukumu juu UAMSHO na vurugu za Huko Unguja hivi karibuni, samahani wote niliowakwaza kwa hilo, nilisukumwa hasa na hamu yangu ya kuona Amani na Utulivu vinatawala nchi hii kwa sababu nayajua madhara yake nikiangalia nchi za wenzetu. Naahidi kufuatilia kwa kina kujua madhumuni ya Uamsho, pengine ni mazuri tu kwa faida ya Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla hata hii habari nitaihariri upya. Wa Billah Tawfik
JibuFuta