Jumapili, 4 Oktoba 2015

MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA AMEFARIKI ALFAJIRI YA LEO BAADA YA KUPATA AJALI YA GARI.

 Marehemu Mtikila alikuwa akitokea mkoani Morogoro kuelekea Dar es salaam kwenye shughuli zake akiwa na gari dogo na watu wengine watatu na gari ilipata ajali majira ya saa 10 alfajiri ya leo. Mchungaji alifariki hapohapo na wenzake wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali. Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa. 
Marehemu Mtikila akiwa eneo la ajali. Marehemu atakumbukwa katika harakati zake za kupigania Taifa la Tanganyika, Mgombea binafsi na haki nyingine nyingi za Binadamu. Mwenyeezi Mungu amlaze mahali pema peponi Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni