Jumapili, 9 Februari 2014

UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA NAMIKANGO NACHINGWEA WAKUTANISHA VIGOGO WA VYAMA MABALIMBALI. MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA LEO.Mwenyekiti wa Chama cha ADC Taifa Bw. Miraji Abdallah pichani katikati.(maktaba)Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Bw. Chikawe yupo naye katika Kampeni.


Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Lipumba juzi alifanya kampeni kumnadi Mgombea Udiwani wake.

Nachingwea, Lindi.
Vigogo wa Vyama mbalimbali vya siasa nchini ikiwemo CCM, CUF,CHADEMA na ADC walimiminika wilayani hapa takribani juma zima lililopita kwa minajiri ya kunadi wagombea wa vyama vyao wa kiti cha Udiwani cha kata ya Namikango, Nachingwea ambacho kipo wazi kwa mwaka mzima sasa baada ya aliyekuwa Diwani wake kufariki mwezi Aprili mwaka jana.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi huo Bw. Kwembe ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, uchaguzi huo utafanyika leo Jumapili tarehe 09/02/2014 kuanzia asubuhi hii hadi saa 10 jioni. Aliongeza kuwa wote watakaokuwa kwenye foleni kufikia muda huo watapiga kura ila watakaofika baada ya muda huo watakuwa wamechelewa, hali ni shwari hadi sasa.
Bw. Miraji Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa ADC aliwasili juzi mjini hapa na jana alifanya mkutano wa kampeni kijijini Namikango, Bw. Freeman Mbowe alitarajiwa juzi na Bw. Chikawe yupo kwa wiki nzima sasa akifanya kampeni za chini kwa chini pia Prof. Lipumba alifanya kampeni na mkutano wa kuimarisha chama hapa mjini Nachingwea. Kwa matokeo ya Uchaguzi wa leo pitia hapa baada ya saa kumi jioni.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni