Jumapili, 3 Februari 2013

MOHAMMED MORSI RAIS WA MISRI ASHINDWA KUFAIDI MATUNDA YA MAPINDUZI, IKULU YALINDWA DHIDI YA WAANDAMANAJI.

Askari wa kupambana na fujo wa Misri wamewekwa kwa wingi nje ya ikulu ya rais mjini Cairo baada ya mapambano ya Ijumaa usiku baina ya wanajeshi na waandamanaji waliowatupia mabomu ya petroli.

Walinzi nje ya ikulu ya rais mjini Cairo

Muandamanaji mmoja alikufa baada ya kupigwa risasi na zaidi ya 50 walijeruhiwa.
Maandamano hayo ambayo piya yalifanywa katika miji mengine kadha ya Misri, ndio ya karibuni kabisa katika mfulululizo wa maandamano ya kumpinga Rais Mohammed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood.
Upinzani unamlaumu kuwa amepindukia madaraka yake.
Televisheni imeonesha matokeo ya maandamano ya jana usiku, mawe na takataka zimejaa mabarabarani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni