Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo FLOLAH TALENT. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo FLOLAH TALENT. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 14 Novemba 2012

KIKWETE ASHINDA KWA KISHINDO UENYEKITI WA CCM TAIFA KWA MSIMU WA HADI 2017, KURA 2 KATI YA 2397 ZASEMA HAPANA.

Rais Jakaya Kikwete amechaguliwa na kushinda kwa kishindo uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM taifa kwa kupata kura 2395.kati ya 2397 zilizopigwa hapo jana mjini Dodoma. Kwa matokeo hayo Ndugu Jakaya Kikwete ameitetea vyema nafasi yake hiyo hadi mwaka 2017. Huku kura za hapana zikiwa 2. Ushindi huo ni sawa na asilimia 99.92.
 
Aidha wagombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambazo kwa upande wa Bara ilikuwa ikigombewa na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Philip Mangula naye amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwa kura 2397,  huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar ameshinda Rais wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein kwa kupata kura zote zilizopigwa 2397. Ushindi wa Shein na Mangula ni sawa na asilimia 100.

Jumatatu, 19 Septemba 2011

SHUKURANI KWA WASAMARIA WEMA


Ndugu Watanzania,



Shukrani za pekee ziwaendee wale wote aliojitolea kwa hali na mali kumchangia mtoto Sesilia Edward ambaye anahitaji msaada wa haraka wa operesheni ya moyo.


Tunapenda kuwataarifu kuwa fedha za operesheni zimekwishapatikana, na tayari tiketi mbili (ya kwake na mlezi wake Peter Nyambaliko) zimekwisha patikana.



Kwa sasa, motto Sesilia amelazwa katika hopsitali ya Regency chini ya uangalizi mkubwa wa Daktari Bingwa Dr. Kanabar na timu yake tayari kupunguza maji yalioyojaa tumboni kabla ya yeye kusafiri siku ya Jumatano.



Dola 6,100 tayari zimekwishalipwa kwa ajili ya matibabu India, na tiketi mbili zimekwishalipiwa. Tayari tumelipa shilingi 200,000 kama admission fee katika hospitali ya Regency ambapo tunatemegemea mtoto Sesilia atalazwa hadi Jumanne tarehe 20, kabla ya kusafiri Jumatano. Gharama zilizobaki za Regency zitagaramiwa na hospitali ya Regency. Yote hii ni katika kuiweka hali yake sawia kabla ya safari ndefu kuelekea India.



Bado tunahitaji msaada wa fedha za kununua madawa ambapo kwa wiki mtoto Sesilia hutumia madawa zaidi ya shilingi 50,000. Tunahitaji nguo kubwa kubwa za kuvaa kwani tumbo linaongezeka sentimeta moja kila baada ya masaa 72.  



Unaweza kumtemebelea mtoto Sesilia katika hospitali ya Regency kwa  leo jumatatu na kesho jumanne



Kama una msaada wa haraka kama nguo, chakula peleka katika kituo cha Chanel Ten – Dar es Salaam.

Na weka pesa katika account zuatazo:



Tigo Pesa:-  0715 095797

MPESA:  –  0762 962467

NMB Account: 2072517079



Kwa maelezo zaidi, piga simu 0767-262625



Watanzania tumeweza, tunamuombea mtoto Sesilia aende salama na arudi salama.

Shukrani za dhati kwenu wote kwa niaba ya Africa Media Group Limited



Hoyce Temu
Mtangazaji  - Mimi na Tanzania