Jumapili, 27 Aprili 2014

MIAKA HAMSINI YA MUUNGANO NA MABADILIKO YA MIELEKEO YA BARABARA ZA SAMORA NA SOKOINE JIJINI DAR KUANZA KESHO, APRILI 28, 2014


 Viongozi wakijadiliana wakati wa zoezi la kuweka Alama muhimu za barabarani Katikati ya Jiji tayari kwa mabadikiko ya mielekeo ya barabara za Samora na Sokoine unaoanza Jumatatu 28/04/2014. 
 Vijana wakiweka kibao cha alama barabarani.
Jana Aprili 26, 2014 zoezi la kuweka Alama muhimu Katikati ya Jiji la Dar es Salaam limekamilika tayari kwa mabadikiko ya mielekeo ya barabara za Samora na Sokoine unaoanza Jumatatu 28/04/2014. Kwa daladala itakuwa kama ifuatavyo:

Habari na Picha na Deo Mutta, DART

1. Daladala Zote zinazotokea Barabara ya Ally Hassan Mwinyi zitaingia mjini kupitia Bibi Titi na kukata kushoto kuingia barabara ya Maktaba na kuishia Posta Mpya na kutoka kwa kuzunguka Mnara wa Askari na kushuka na Maktaba na Kupinda kulia kuingia Bibi Titi na baadaye Alli Hassan Mwinyi.

2. Daladala Zote zinazotokea Barabara ya Morogoro zitapinda kushoto kuingia Bibi Titi na Kupinda kulia kuingia Maktaba hadi Posta Mpya. Zitatoka kwa kuzunguka Mnara wa Askari na kuingia Samora hadi Clock Tower na kuingia Uhuru na Kupinda kulia kuingia Bibi Titi na Kupinda kushoto kuingia Morogoro.

3. Daladala zinazotokea Barabara ya Uhuru zitakwenda moja kwa moja hadi Clock Tower na kuingia Barabara ya Railway na Kupinda kushoto kuingia Sokoine na kuishia Stesheni. Zitatoka kwa kupitia Samora kutokea station na kuingia Uhuru kupitia mnazi mmoja.

4. Daladala zinazotokea Barabara ya Nyerere zitapita Bibi Titi na kukunja kulia kuingia Uhuru hadi Clock Tower na kuingia Railway na kukunja kushoto kuingia Sokoine na kuishia Stesheni. Zitatoka kupitia Samora hadi Clock Tower na kuingia Nkurumah na kuingia Nyerere eneo la Cocabs.

5. Daladala zinazotokea barabara ya Kilwa Zitapitia Sokoine na kuishia Stesheni na kutoka kupitia Railway na kuingia Sokoine kuelekea Water Front.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni