Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akipima kwa tape maalum urefu wa moja ya barabara zilizojengwa na Manispaa ya Sumbawanga katika Mji huo kuhakikisha kama barabara hiyo imejengwa kwa vipimo vilivyoanishwa kwenye mpango wa ujenzi huo (BOQ). Naibu Waziri huyo alitumia fursa hiyo kuziasa halmashauri zote nchini kusimamia vyema fedha za Serikali katika miradi kuhakikisha inafanana na thamani ya fedha zilizotumika, alilazimika kusema hayo baada ya kubaini mapungufu mbalimbali katika mradi huo wa barabara na miradi mingine aliyofanikiwa kuitembelea Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akikagua barabara za lami zilizo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga zilizojengwa hivi karibuni. Katika ukaguzi huo alibaini mapungufu mbalimbali katika ujenzi huo na kuagiza Halmashauri hiyo kuhakikisha mapungufu hayo yanaondolewa. Aliitaka pia halmshauri hiyo kusimamia vyema kazi za Serikali kuepusha minong’ono inayotoka kwa wananchi juu ya utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji Serikalini.
CREDITS; RUKWAREVIEW
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni