Ole Millya, aliyekuwa Mwenyekiti wa UV-CCM Arusha kabla ya kujiuzulu leo mchana
Taarifa ya TBC ya saa saba mchana huu imeripoti, aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Arusha (UV-CCM) tangu 2008, James ole Millya amejivua nyadhifa zake zote kutoka chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).Millya amerekodiwa na waandishi wa habari katika hoteli ya Kibo Palace alipozungumza nao akisema kuwa hatatoa sababu za kina za kujing'atua CCM kwa wakati huu mpaka siku chache zijazo.
Ole Millya alikuwa pia Mjumbe Kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM-Mkoa.
Alienguliwa hivi karibuni katika harakati zake za kuwania Ubunge wa Afrika Mashariki kupitia CCM.
Katibu wa Itikadi na Uenezi, CCM-Taifa, Nape Nnauye kwenye facebook.com/nape.nnauye amesema: Nampongeza Millya kwa kuamua kukisaidia Chama Changu, kwani alishakuwa mzigo mkubwa kwa CCM. Itakumbukwa alikuwa afukuzwe kwenye chama kutokana na mambo alokuwa akifanya. Akapewa KARIPIO ili apate muda wa kurekebisha tabia yake! Kaondoka akiwa chini ya karipio. Kajivua gamba, tunampongeza kwa kuitikia wito wa kujivua gamba. Kila lakheri aendako ni kijana bado anayo mengi ya kujifunza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni