KATIBA NI NINI?
Katiba ya nchi ni mkataba wa namna nchi itakavyoendeshwa ikizingatia masuala makuu ya msingi ikiwemo haki za raia,namna uongozi wa nchi utakavyopatikana, vipaumbele vya taifa mila na desturi za watu wa taifa husika. Mkataba huu ni kati ya wananchi na kikundi cha wananchi wachache walioteuliwa kuongoza wenzao.(viongozi)
Wananchi wanakubali kutoa madaraka ya kuongoza nchi yao kwa viongozi wao(serikali) ili watekeleze makubaliano yaliyomo ndani ya katiba kwa kufuata vigezo mbalimbali mfano serikari ikishindwa kuongoza vizuri basi itabidi iachie madaraka na wawekwe wengine watakaotekeleza mkataba ule.(katiba)
Hivyo basi watawaliwa wanajitoa na kukubali kukabidhi madaraka ya kuongozwa kwa kikundi kidogo cha watawala(dola) ambacho kina watu toka jamii ileile, ndio maana tunaita mkataba. Katiba ni sheria mama, mambo yote yatakayotekelezwa au sheria zitakazotungwa itabidi zifuate matakwa ya katiba ile, yasiwe kinyume. Mfano katiba ikisema; "Ardhi ni mali ya Rais wa Nchi, kila mwananchi ana haki ya kumiliki ardhi." Basi kusitokee itakayosema vinginevyo kama, Matajiri au mtu mmoja anaweza kumiliki ardhi kubwa na kuihodhi wakati wananchi wengine hawana hata kipande cha kulima bustani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni