Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAISHANIVITA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAISHANIVITA. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 13 Aprili 2012

TIMU YA MAJIMAJI YAMSHUKURU MKUU WA MKOA WA RUVUMA KWA KUINUSURU ISIFE.

 
                                MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU

NA STEPHANO MANGO,SONGEA
UONGOZI wa klabu ya Majimaji ya Songea imetoa pongezi ya kumshukuru Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu kwa kazi kubwa ya kuiwezesha  timu hiyo kubakia ligi ya Daraja la kwanza kwa ngazi ya Taifa msimu huu.
Akizumgumza mjini hapa  ,Katibu Msaidizi wa Wanalizombe hao, Zakaria Ndumbaro alisema kuwa uongozi wa Majimaji umeweza kumwandikia  barua ya kumpongeza pamoja na kumshukuru  juu ya mchango wa kifedha , fikra na busara zake ambazo  ndizo zilizoiwezesha timu hiyo kubakia kucheza tena ligi hiyo msimu ujao.
Alisema kama siyo mkuu wa mkoa kuipiga jeki timu hiyo basi kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kushuka daraja na kucheza ligi ya mkoa kitu ambacho kingekuwa fedheha kwa timu kama hiyo yenye historia ya soka hapa nchini.
Alisema katika kipindi chote cha ligi hiyo ya Daraja la kwanza kwa ngazi ya Taifa hatua ya makundi, licha ya kukabiliwa na tatizo la uongozi na kupelekea wanachama kuwaengua baadhi ya viongozi na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mohamed Gayo kujihuzuru timu hiyo ilifikia hatua ya kuyumba na hata kutiliwa shaka kushiriki ligi hiyo.
 Alisema kutokana na busara za mkuu huyo aliweza kuunganisha nguvu ya pamoja baina ya viongozi waliokuwepo madarakani, wanachama na wale walioenguliwa na kuwa kitu kimoja na kufanikiwa kucheza na kubakia katika hatua hiyo licha ya matatizo ambayo waliweza kukumbana nayo katika kipindi hicho cha ligi.
 Alisema kutokana na matatizo yote hayo ambayo waliweza kukabiliana nayo, tayari uongozi wa timu hiyo umeanza kujipanga kuhakikisha na timu hiyo itaendeshwa kwa mtindo wa mfumo wa  kibiashara na kuachana na mfumo wa sasa wa timu kuendeshwa na wanachama kwa kutegemea mifuko yao.
 Alisema katika kuhakikisha heshima ya timu hiyo inarejea  kama ilivyo katika miaka ya nyuma  tayari amedai wameandaa mazingira mazuri ikiwemo ya kufanya mkutano wa pamoja kati ya wadau na wanachama  mada kuu kuelezea changamoto zinazoikabili pamoja na maendeleo yake kwa kipindi cha miaka mitatu ya nyuma na malengo wanayokusudia  kwa miaka ya mbele.
 Pia, Ndumbaro alisema katika kikao chao walichokutana hivi karibuni wameweza kumsimamisha kazi Ofisa Habari wa Klabu ya Majimaji, Osama Ulaya kwa kile alichokidai amekuwa akifanyakazi kinyume na maadili ya kazi yake na kupelekea timu hiyo kwa kipindi chote  kuingia katika malumbano yaliyochangia na kuwepo kwa uvumi na habari za uchochezi ambazo zilikuwa zikitolewa na Ofisa huyo.
 MWISHO

Jumamosi, 11 Februari 2012

JAMANI TUNAKOKWENDA NI HUKU AU TUMEKOSEA, MAUAJI YA KUTISHA HUKO SONGEA.

Majambazi wawili wachomwa moto wakiwa hai

Pichani ni miili ya watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi  ambao walipigwa na  kuchomwa moto hadi kifo katika eneo la Ruhuwiko manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Baadhi ya wakazi wa eneo la Ruhuwiko ambao hawakutaka kutaja majina yao walidai kuwa kabla ya tukio hilo watu hao hawakuweza kufahamika majina yao waliwasili eneo hilo majira ya saa tatu asubuhi wakiwa na lengo la kuuwa na kuondoa viungo vya uzazi vya binadamu ambavyo inadaiwa vinauzwa kwa fedha nyingi.


Wananchi hao walidai kuwa watu hao walifika kwa mama mmoja ambao walidai wanamtafuta hatimaye wakiwa wanakunywa katika klabu moja ya pombe za kienyeji inadaiwa wakazi wa eneo hilo waliwatilia mashaka watu hao na kuaanza kuwahoji ambapo inadaiwa baada ya kupata kipigo na kuanza kuchomwa walieleza kwamba wao ni wauaji na walipewa fedha kwa ajili ya kuuwa na kwamba tayari wamekuwa wamefanya matukio kadhaa ya mauaji .

Chanzo cha habari kimebainisha kuwa wauaji hao walidai kuwa wapo 50 na wanatakiwa kuuwa watu zaidi ya 100 wakiwemo wanaume 60 na wanawake 40 kwa kuwaondoa sehemu zao za siri ambazo inadaiwa ni biashara ambayo inawapatia fedha nyingi .

Baada ya wauaji hao ambao walikutwa na shilingi 500,000 kukiri kuwa kazi yao ni kuuwa ndipo wananchi wengi wenye hasira waliamua kuanza kuwapa kipigo kizito kisha kununua petroli na kuanza kuwachoma wakiwa hai .Hadi polisi wanafika katika eneo hilo miili ya watu hao ilikuwa inaendelea kuungua kwa moto.

Uchunguzi umebaini kuwa wakazi wa Ruhuwiko waliamua kuchukua sheria mkononi baada ya matukio ya uharifu na  mauaji kujitokeza katika eneo hilo  na kwamba hii ni mara ya pili kwa wakazi wa Ruhuwiko kufanya mauaji ya kutisha ambapo miaka 25 iliyopita watu wengine wawili waliodaiwa kuwa ni majambazi sugu waliuwa na kisha miili yao kuchomwa moto.
"Mimi binfasi nimefurahia sana kitendo hiki labda sasa majambazi yataogopa kuendelea kufanya uharifu katika eneo hili,hivi sasa hatuna amani kabisa wizi imekuwa ni jambo la karibu kila siku ,mauaji nayo yanazidi kuendelea ,waharifu wengine wanakamatwa na kuachiwa  acha wananchi wajichukulie sheria mkononi'',alisema mama mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na polisi bado wanaendelea na uchunguzi.
albano.midelo@gmail.com