Jumamosi, 4 Januari 2014

MAREHEMU MGIMWA KUZIKWA JUMATATU HUKO IRINGA.

Waziri wa Fedha wa Tanzania William Mgimwa, ambaye alifariki siku ya Jumatano kwa sababu za kawaida katika hospitali moja huko Afrika ya Kusini, anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu (tarehe 6 Januari), gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti.

Marehemu William Mgimwa.

Mwili wa Mgimwa unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam siku ya Jumamosi, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, William Lukuvi.Mgimwa alifariki katika hospitali ya Mediclinic Kloof ya Pretoria baada ya kulazwa kwa matibabu ya dharura. Mwezi huu angetimia miaka 64.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, Mh. William Lukuvi(Mb)
Siku ya Jumapili, mwili wa Mgimwa utapelekwa Ukumbi wa Karimjee, ambako maafisa na wananchi watatoa heshima zao za mwisho, ikifuatiwa na sala maalumu, Lukuvi aliwaambia waandishi wa habari.
Mgimwa, mkongwe wa Benki ya Taifa ya Biashara ya Tanzania, alichaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010 na kuteuliwa waziri wa fedha mwaka 2012 na ilisifika kwa kuongoza jitihada za Tanzania za kutafuta masoko ya dhamana ya kimataifa ili kugharamia uwekezaji na kukabiliana na umaskini, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni