Jumanne, 2 Desemba 2014

KINANA AFANYA KUFURU YA CCM MIKOA YA KUSINI. ACHOTA WANACHAMA WAPYA KWA MAELFU.



MKUTANO WA HADHARA MTWARA MJINI
Wakazi wa Mtwara mjini wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mtwara mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kazi ya CCM ni kuisimamia Serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mtwara mjini na kuwaa
 Mbunge wa Mtwara Mjini Ndugu Hasnain Murji akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyotekelezwa vizuri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa ambapo pia alieleza changamoto zinazowakabili wananchi wa Mtwara mjini hivyo kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kusaidia katika kufanikisha baadhi ya mambo ambayo yameonekana kukwamishwa na viongozi wa juu serikalini.

 Wananchi wakilizunguka gari alilopanda Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza kuhutubia kwenye viwanja vya Mashujaa Mtwara mjini.

MAPOKEZI YA KINANA MTWARA MJINI
  Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
     Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji.
                                                   MTWARA VIJIJINI 
 Wananchi wa kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji hicho kinachopakana na nchi ya Msumbiji.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kitaya kilichopo mpakani na nchi ya Msumbiji ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara ambapo anakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kujenga na kuimarisha chama.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Nanguruwe ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna sheria zinazomkandamiza mkulima inabidi zitazamwe upya kwani zisipobadilishwa mkulima atakuwa anakandamizwa kila siku na kutoona faida ya kuwa mkulima wa korosho.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Nanguruwe wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM kwenye wilaya ya Mtwara Vijijini,tarehe 28 Novemba 2014.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mnara wa shujaa Ahamad Mzee aliyepambana na Wareno waliokuwa wanataka kuivamia Tanzania mwaka 1972 mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
                                                          TANDAHIMBA 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa zao la korosho lina hadithi nyingi sana na njia pekee ya kuleta ukombozi kwa mkulima ni kujenga kwa viwanda vya kutosha vya kubangulia Korosho nchini pia aliwataka wazazi wa Tandahimba kusisitiza elimu kwa watoto wao kwani ndio mkombozi pekee atakayekuja kuwakomboa kwenye maisha yao.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wasihadaike na wapinzani ambao muda wao wa ujana wameutumia wakiwa CCM na uzeeni kuingia upinzani na kuanza kuhadaa watu walioishi kwa amani kwa muda mrefu.
  Wananchi wa Tandahimba mkoani Mtwara wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anazunguka nchi nzima kukagua na kuimarisha uhai wa Chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Mndimba wakati waujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba wilayani Tandahimba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani kata ya Mdimba wilaya ya Tandahimba.
                                                   NEWALA 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaonyesha wananchi wa Mkwedu kadi ya CUF iliyorejeshwa kwake na Hakika Ibrahim ambaye alirudisha kadi hiyo baada ya kuona na kuelewa utekelezaji wa ahadi za CCM unavyokwenda vizuri.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionnyesha kadi juu zilizorudi kutoka upinzani ambapo wanachama hao kutoka upinzani wameahidi kushirikiana na CCM kwa ajili ya kuleta maendeleo yaTengulengu wilayani Newala.
 Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akivua nguo za Chadema mbele ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye.
 Wananchi wakishangilia kurejea kwa  Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona kwenye mkutano wa hadhara uuliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Newala
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Newala kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali lazima itafute namna ya kuhakikisha uzalishaji wa korosho wote unafanyika nchini kwa kujenga viwanda vya kutosha vya korosho.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akiwa amekabidhi kadi yake na ya mkewe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
                                                       NANYUMBU 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mangaka  wilaya ya Nanyumbu ambapo aliwaambia CCM ya sasa itakuwa kali kuliko wakati wowote na itaisimamia serikali na kuipongeza inapofanya vizuri na itakapofanya vibaya itasemwa.
  Wananchi wakimfurahia kumuona mkuu wao mpya wa mkoa.
                                                          LULINDI 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe ambapo alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150 kata ya Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
 Wananchi wa Kijiji cha Machombe wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea nchi nzima kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la maji akiongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Farida Mgomi pamoaja na wanakijiji cha Machombe kata ya Marika.
 Kadi zilizorudishwa kutoka kwa wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari yao leo wamerudi na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi.
 Wanachama wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
                                                      MASASI MJINI 
 Wanachama wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
 Wana CCM wakishangilia kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa fisi wilayani Masasi.
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Masasi kwenye uwanja wa Fisi na kuwataka Watanzania kukiamini chama chao .
  Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo mjini Masasi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Masasi ambapo aliwaambia viongozi wajenge utaratibu wa kuwaeleza wananchi maendeleo yao na yapi yamefanikiwa na wapi hawajafanikiwa, wapi yanakwamishwa.
                           MKUTANO WA HADHARA  LINDI MJINI
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni chama pekee chenye mfumo ulioanzia chini hivyo watu waache unyonge Serikali hii ni ya CCM.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi wa Lindi ni muda wa kuwaondoa wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba mwaka huu kwa kuipigia kura CCM.
                                                       RUANGWA 
 Mapokezi ya Kinana jimbo la Ruangwa
 Wananchi wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara.
 Wananchi wa Ruangwa wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kujenga na kukiimarisha chama,Katibu Mkuu wa CCM ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Ruangwa waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Kinana amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kuzunguka nchi nzima ,kushiriki kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo,kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hasa ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.
  Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo alielezea katika kipindi chake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge ameshiriki shughuli mbali mbali za maendeleo jimboni kwake.
                                                        LIWALE  
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia kuwa wapinzani kwenye mikoa hiyo hawajai hata kiganjani hivyo wananchi wasipoteze muda kwa wapinzani.
 Wananchi wa Liwale wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi                                                      NACHINGWEA
  Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia upinzani umepotea kabisa hivyo wasipoteze muda wao kushabikia
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia kuwa CCM itakuwa wakali pindi serikali inapokosea mambo na kuchelewa kuchukua hatua, kwani maumivu na mateso wanapata wananchi, akizungumzia kusikitishwa kwake kwenye viwanda vya korosho ambavyo vimegeuzwa kuwa maghala na hakuna mtu serikalini amestuka kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
                                                  MTAMA 
 Katibu wa NEC Itiakdi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Chiuta ambapo aliwaambia Chiuta ni nyumbani na aliwataka watu wachukue tahadhari na vyama visivyo na sera wala dira
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Chuta ambapo aliwaambia kuwa maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi na kujituma, ambapo aliwaambia kila nchi itaendelezwa na watu wake.
                                                               MCHINGA 
 Katibu wa Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mchinga mkoani Lindi

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi wa Mchinga.
                                                 KILWA KUSINI 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko ambapo aliwaambia watendaji wa serikali kutoa elimu ya kuwafahamisha wavuvi kabla ya kuchukua maamuzi ya kuchoma vifaa vyao vya kazi,pia aliwaambia wananchi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi kitajirekebisha makosa yake na kuhakikisha kinashinda kwa kishindo kwenye chaguzi zijazo kwani jimbo la kusini Kilwa limepotea kutokana na migongano ndani ya CCM, hivyo basi uchaguzi ujao tujipange vizuri na kurudisha jimbo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko ambapo aliwaambia kuwa wapinzani hawasemi ukweli unaoendelea kwenye vyama vyao havisemi kama vimekufa.
Mwananchi akishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa.
                                                         
  Umati wa wakazi wa kata ya Chumo wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Chumo kwenye viwanja vya shule ya msingi Chumo na kuwaambia kuwa huu si muda tena wa kuwasikiliza wapinzani kwani upinzani ulishaisha nchini hivyo .



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Chumo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chumo ikiwa siku ya kwanza ya kuanza ziara yake ya mikoa miwili ya Lindi na Mtwara.
Credits. kamerayangublog

Jumanne, 11 Novemba 2014

MBOWE AMCHANA SITTA MBELE YA WAPIGA KURA WAKE.

Mbowe ‘amwaga sumu’ nyumbani kwa Sitta

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwasili kwenye Uwanja wa Extended mjini Urambo, Tabora alikohutubia mkutano wa hadhara juzi. Na Mpigapicha Maalum
Urambo. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa Urambo Mashariki na kumshutumu Mbunge wa jimbo hilo, Samuel Sitta kwa kuchakachua maoni ya wananchi katika mchakato wa Katiba Mpya.
Katika mkutano huo ulifanyika katika Uwanja wa Extended mjini hapa takriban mita 100 kutoka nyumbani kwa Sitta aliyeongoza Bunge la Katiba, Mbowe alisema historia ya nchi hii itamhukumu mbunge huyo kwa maovu hayo.
Alisema kutokana na uovu huo wa Sitta ambaye amekuwa akiisifia Katiba Inayopendekezwa kuwa itakuwa nzuri Afrika Mashariki na Kati, vyama vya upinzani vitaendelea kuidai katiba ya wananchi hata kwa miaka 100 ijayo.
Aprili mwaka huu, wabunge wa vyama vya upinzani chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walisusia Bunge la Katiba mjini Dodoma wakilalamikia kuvunjwa kwa kanuni na kutofuatwa kwa mapendekezo ya wananchi yaliyotolewa katika Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho kwenye Operesheni Delete CCM, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema ana uhakika Sitta ataipata hukumu hiyo ya historia kwa kile alichosema kudhulumu haki ya Watanzania milioni 45.
Mbowe anayetumia chopa katika ziara hiyo, alifika katika uwanja huo saa 11.45 na kuhutubia kwa dakika 30.
“Mzee Sitta najua upo nyumbani hapo na unanisikia, kama hunisikii basi mke wako Mama Margreth Sitta atakuwa ananisikia, lakini kama naye hayupo basi kutakuwa na wahudumu watanisikia na watakuja kukueleza,” alisema huku akiwaonyesha wafuasi wa chama hicho nyumba ya Sitta iliyopo jirani na uwanja huo.
Alisema Sitta alipuuza maoni ya wananchi waliyotoa katika mchakato wa Katiba Mpya na ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba badala yake akaweka maoni ya chama chake cha CCM.
“Tunasema kwamba historia ya nchi hii itamhukumu kwa maovu aliyoyafanya kukataa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya chama chake,” alisema.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, alisema baada ya maoni ya wananchi kuchakachuliwa... “Sasa tutaidai Katiba Mpya hata kwa miaka 100 ijayo.”
Alisema wabunge wa vyama vya upinzani walimwamini Sitta kwa kumpigia debe na baadaye walimpa kura  iliyomfanya awe Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kutokana na rekodi yake alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Tulifanya hivyo kwa kumwamini kutokana na rekodi zake akiwa spika, tunajuta kumchagua hatukufahamu kwamba atatusaliti na kudhulumu haki za Watanzania,” alisema Mbowe.

Alhamisi, 6 Novemba 2014

WATALII WALALAMIKIA RUSHWA KATIKA VIZUIZI VYA BARABARANI HUKO ZANZIBAR.



KAMA vituo 66 vya treni havitoshi katika safari nzima ya utalii, Teresa Williamson wa  Australia na Annemarie Schuller wa Uholanzi wamesema Watanzania wanaishi katika mazingira magumu na wanastahili kubadilika.
 Kauli hiyo wameitoa wakati wakizungumza na Mwandishi wa makala haya muda mfupi kabla ya kuondoka kurejea makwao baada ya ziara ya wiki mbili katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika ziara yao ya kitalii walitumia treni, barabara na maji tena kwa kutumia jahazi wakitokea Pangani Tanga hadi Zanzibar.
Nilitaka kujua baada ya utalii wao wameona nini nchini Tanzania walisema pamoja na kufanikiwa kuwaona wanyama wakubwa watano kama walivyofikiria wakati wakiwa makwao wameshuhudia maisha masikini zaidi kuliko matarajio.
“Sijui inatokeaje watu wengi wana simu za mkono lakini ukiangalia maisha yao unayaona kuwa magumu sana,” alisema Teresa ambaye alifafanua kwamba ugumu wa maisha unaonekana katika miundombinu na usafirishaji, ulaji na utunzaji wa mazingira.
Wakiwa wamezaliwa mjini hawakuwa wanajua vijijini kukoje mpaka walipofika nchini Tanzania na kukumbana na hali ambayo hawakuitarajia  hata kidogo.
Pamoja na kushuhudia matukio yasiyokuwa ya kawaida katika safari na mbugani ugumu wa maisha ambao wao wataendelea kuangalia ni mawasiliano, usafirishaji, na usalama.
Wamesema katika safari yao wamekumbana na tatizo  kubwa la chakula, usahihi wa taarifa na tatizo la mawasiliano.
“Pamoja na wananchi kuwa marafiki tumeona tatizo kubwa la usafiri na aina ya chakula kinacholiwa na usafi,” alisema Schuller ambaye kitaalamu ni mganga wa meno.
Kwa mtazamo wa watalii hao taifa hili linahitaji kubadili wananchi wake kwa kuwapa elimu ya kutosha kuhusu mazingira yanayowazunguka hasa kwa kujali aina ya mlo wanaokula, usafi wa mazingira na kujali gharama kwa huduma wanazotoa kwa wageni.
Teresa alisema kwa kuwa na aina moja ya chakula Ugali na wali muda wote bila maziwa mboga za majini kunatengeneza aina ya udumavu ambao unachochea watu kukosa lishe bora.
“Tumekuwa tukikumbana na chakula cha aina ile ile kila mahali tunapoenda, chakula cha nafaka ambacho ni wanga lakini hukutani na matunda, mboga za kijani na maziwa,” alisema Teresa.
Pamoja na kuzungumzia mlo, wageni hao walizungumzia  tatizo la rushwa na kusema walipokuwa Zanzibar pamoja na kuhisi kwamba ulinzi ni mkali kutokana na kusimamishwa kila mara katika gari, lakini waliona kuna kitu si sahihi wakati wa mazungumzo kati ya dereva na askari.
“Pale tuliona shida kidogo kwanini wanapenyeza mkono tena unaona kwa uangalifu mkubwa?” Alisema  Annemarie ambaye alisema matendo waliyokumbana nayo yanatia wasiwasi hasa unaposimamishwa mara saba katika kipindi cha dakika 40 wakati wakiwa kisiwa cha Zanzibar.
Kwao wanaamini kwamba lipo tatizo la rushwa na pia tatizo la lugha kwani wengi wameshindwa kuwasiliana nao kutokana na shida ya lugha kiasi ya kwamba wapo watu walikuwa wanawakwepa kwa sababu hawaelewani na wakati mwingine walifanya maamuzi ambayo hayakuwa sahihi kutokana na lugha gongana.
Anasema walipofika Tanga waliambiwa wanaweza kufika Zanzibar kupitia Pangani.Walisema usafiri uliwachosha na hata walipofika Pangani wakagundua kwamba mawasiliano si sahihi lakini wakaingia katika boti na kuelekea Zanzibar.
Boti hiyo ambayo ilikuwa kila mara inatolewa maji, iliwaogopesha sana lakini hata walipokuwa wakitaka kujua wanajiokoaje walijikuta wakiambulia kuambiwa kwamba njia za kujiokolea ni palepale walipo.
Hata hivyo walifarijika baada ya kugundua maboya ya kujiokolea ndio waliyoyakalia.
Pamoja na kufurahishwa na matembezi yao hasa kwa kuona kwamba wameweza kuwaona wanyama wakubwa kama tembo, chui, simba, faru,twiga na nyati walisema ipo haja ya kupunguzwa kwa kiingilio kwani kwa sasa wanakiona kama ghali.
Nilipomuuliza kuhusu Serengeti kama itakufa, alisema kwamba hadhani kwani anaona kwamba bado haijavurugwa sana na kama Watanzania watakubali kwamba ile ni mali yao haitakufa.
“Ni suala la kuelimika na kuhakikisha kwamba utamaduni unajali mazingira, unajali afya na wajibu,” alisema Teresa ambaye katika miaka yake 55 alisema Afrika bado ni bara la kutembelea.
Alisema walifika Sumve kuwaona jamaa zao na marafiki, lakini walishangazwa na wingi wa vituo ambapo treni inasimama japo waliona kwamba hali ile inaweza kuwa inasaidia mzunguko sahihi wa uchumi  wa eneo hilo.
“Njiani tuliona mengi lakini nadhani baya kabisa ni watu kutokujali mazingira yao. Uchafu unatupwa kila mahali na hata maeneo mengine hayakuwa na vyoo na yale yaliyokuwa na vyoo hata karatasi laini za chooni zilikosekana,” alisema Teresa.
Kwa maneno yao watu wanatakiwa kubadilika kupitia elimu ili kutambua kwamba kuna haja ya kuwa na mazingira safi kwa manufaa yao na kizazi kijacho.
“Unakosaje mahali pa kujisaidia? Umelipa fedha ili ufurahi inakuaje unapokosa huduma,” aliuliza Teresa.
Kwa maneno yao wenyewe ugumu wa kupata huduma inayoridhisha kwa fedha halisi  si tu katika maeneo waliyofikia bali hata katika usafiri.
“Ukiwa peke yako huwezi kufanikiwa,” alisema Teresa na kuungwa mkono na Annemarie ambaye yeye kuja Afrika ilikuwa mara yake ya kwanza. Moja ya tatizo ni kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu wanaoandaa usafiri ambao wamekuwa wakiwatoza ada kubwa kuliko wanayokuja kujua baadaye.
Yalikuwa ni maoni ya mwandishi wa makala haya kwamba tatizo hilo linatokana na kutumia wakala katika masuala ya utalii na badala yake watu  ambao wamejitangaza kujua Tanzania na kwamba watawapokea.
Watu hao ambao unaweza kulinganisha na vishoka wanachojali wao ni kuongeza cha juu na kuwafikisha watalii wao katika maeneo ambayo ni rahisi na wakati mwingine bila kuwa na muunganisho mwema.
Pamoja na udhaifu katika masuala ya utalii hasa mawasiliano na upashanaji wa taarifa elimu inayotakiwa miongoni mwa wananchi ni kubadili masuala yao yanayowafanya wawe na maisha magumu.
Kwa watalii hao wamesema hawajawahi kuona ardhi yenye rutuba kubwa kama Tanzania na kinachotakiwa kufanywa ni watu wake kutumia fursa zilizopo kujikwamua katika dhiki ya umasikini na kuboresha maisha yao.
Walielezea kufurahishwa na ukarimu uliofanywa na Wapare walipoenda kutembelea eneo la Mbagha ambako walilala Tona Lodge na kupata maelezo kuhusu kijiji na kutembelea vivutio mbalimbali likiwemo jiwe lililotumika kuua watoto waliokuwa wanafikiriwa wana mikosi.
Naam, mpaka mwisho wa mazungumzo wageni hao walilalamikia usafi, utunzaji wa mazingira, mfumo wa lishe na mawasiliano hafifu pamoja na lugha gongana unaleta utata wa uaminifu.
Credits; Lukwangule

Jumatatu, 3 Novemba 2014

JAJI WARIOBA APIGWA KIBAO KWENYE MKUTANO UBUNGO PLAZA. ULIITISHWA NA MWALIMU NYERERE FOUNDATION.

TAARIFA YA TUKIO LILILOTOKEA UBUNGO PLAZA  JANA.

IMG-20141102-WA0021
 Mkutano ulifanyika kuanzia saa 1520hrs ukiwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu mh. Joseph Sinde Warioba. Mkutano ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za kisiasa. Mkutano ulirushwa moja kwa moja na ITV na maudhui yake kimtazamo ulilenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya tume ya Warioba na ile ya Mh. Sitta na tume yake. Baada ya Mh. Warioba kuelezea kwamba Muungano sio tunu ila
ni urithi ndipo wakereketwa wa upande wa Mh. Sitta walipoinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya katiba ya Mh. Sitta ambayo wao wameshaikubali? Baada ya mabango yale kuinuliwa yakazua tafrani ambapo walishauriwa kutoyainua kwa sababu haukuwa mkutano wa kisiasa na wakanyang’anywa na kuyachana ndipo vurugu/kashfa/matusi yakaanza kutolewa dhidi ya meza kuu. Hali hii ilisababisha kushikana, kusukumana na kurushiana viti. Katika tafrani hiyo mh. Warioba alipigwa kibao na Mh. Paulo Makonda- ambaye ni katibu wa UVCCM TAIFA. Mtuhumiwa huyu pamoja na wengine wanne wamekamatwa kwa mahojiano. Upelelezi unaendelea na juhudi za kuwapata wengine zinaendelea.