Ijumaa, 23 Oktoba 2015

MAHAKAMA KUU LEO IMEAMUA KUKAA MITA 200 AU ZAIDI BAADA YA KUPIGA KURA HAIRUHUSIWI...


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa uamuzi wa mvutano wa kukaa mita 200 kutoka katika kituo cha kupigia kura na kusema kuwa haruhusiwi mtu yeyote kukaa hata kwenye umbali zaidi ya mita hizo.

Jumapili, 4 Oktoba 2015

MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA AMEFARIKI ALFAJIRI YA LEO BAADA YA KUPATA AJALI YA GARI.

 Marehemu Mtikila alikuwa akitokea mkoani Morogoro kuelekea Dar es salaam kwenye shughuli zake akiwa na gari dogo na watu wengine watatu na gari ilipata ajali majira ya saa 10 alfajiri ya leo. Mchungaji alifariki hapohapo na wenzake wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali. Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa. 
Marehemu Mtikila akiwa eneo la ajali. Marehemu atakumbukwa katika harakati zake za kupigania Taifa la Tanganyika, Mgombea binafsi na haki nyingine nyingi za Binadamu. Mwenyeezi Mungu amlaze mahali pema peponi Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila.