Jumatano, 12 Februari 2014

MAAFISA WAWILI WA TBA WAHUKUMIWA JELA MIAKA TISA KILA MMOJA.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) na mwenzie wamehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela au kulipa faini ya shilingi milioni kumi na tano kila mmoja na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya 2007. Watuhumiwa hao wanadaiwa kwa nyadhifa zao waliidhinisha ujenzi wa jengo la ghorofa 18 katika eneo ambalo mipango miji inaonesha inaruhusiwa kujenga majengo yasiyozidi ghorofa saba tu.

Jumapili, 9 Februari 2014

UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA NAMIKANGO NACHINGWEA WAKUTANISHA VIGOGO WA VYAMA MABALIMBALI. MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA LEO.



Mwenyekiti wa Chama cha ADC Taifa Bw. Miraji Abdallah pichani katikati.(maktaba)



Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Bw. Chikawe yupo naye katika Kampeni.


Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Lipumba juzi alifanya kampeni kumnadi Mgombea Udiwani wake.

Nachingwea, Lindi.
Vigogo wa Vyama mbalimbali vya siasa nchini ikiwemo CCM, CUF,CHADEMA na ADC walimiminika wilayani hapa takribani juma zima lililopita kwa minajiri ya kunadi wagombea wa vyama vyao wa kiti cha Udiwani cha kata ya Namikango, Nachingwea ambacho kipo wazi kwa mwaka mzima sasa baada ya aliyekuwa Diwani wake kufariki mwezi Aprili mwaka jana.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi huo Bw. Kwembe ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, uchaguzi huo utafanyika leo Jumapili tarehe 09/02/2014 kuanzia asubuhi hii hadi saa 10 jioni. Aliongeza kuwa wote watakaokuwa kwenye foleni kufikia muda huo watapiga kura ila watakaofika baada ya muda huo watakuwa wamechelewa, hali ni shwari hadi sasa.
Bw. Miraji Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa ADC aliwasili juzi mjini hapa na jana alifanya mkutano wa kampeni kijijini Namikango, Bw. Freeman Mbowe alitarajiwa juzi na Bw. Chikawe yupo kwa wiki nzima sasa akifanya kampeni za chini kwa chini pia Prof. Lipumba alifanya kampeni na mkutano wa kuimarisha chama hapa mjini Nachingwea. Kwa matokeo ya Uchaguzi wa leo pitia hapa baada ya saa kumi jioni.


Jumapili, 2 Februari 2014

MWENYEKITI WA CCM TAIFA AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO LEO HUKO MBEYA KUADHIMISHA MIAKA 37 YA CCM.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongoza matembezi ya mshikamano kutoka viwanja vya Soweto Kwenda Bustani ya Jiji jijini Mbeya huku akiwa amewashikilia watoto wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM yanayofanyika leo mkoani Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchema, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee Philip Mangula na kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Fedha na Uchumi Mama Zakhia Megji, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi wakishiriki matembezi hayo, Matembezi hayo ya kilomita tano yalianza Saa moja na nusu na kumalizika Saa mbili na robo.
,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kipenzi cha watoto ameshiriki nao katika matembezi hayo kama anavyoonekana akitembea sambamba na watoto hao
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza na wana Mbeya mara baada ya kupokea matembezi hayo kwenye bustani ya Jiji jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha Mapinduzi yanayofanyika kwenye uwanja wa Sokoine leo jijini Mbeya.
2A3Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwasili eneo la Soweto 4Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 5Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa kitaifa wa CCMwakiwa wamejipanga tayari kwa kuanza matembezi hayo. 7,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kulia ,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakisonga mbele. 8Maaskari wa vikosi vya usalama Barabarabi na Usalama wa rais wakijiweka sawa na kuupanga msafara wa matembezi hayo 9Wanahabari wakishiriki katika matembezi hayo 10Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kulia akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza barabarani wakati matembezi hayo yakiendelea. 11Adam Gille na wanahabari wengine wakiwajibika kama kawa 12Wananchi wakishiriki katika matembezi hayo 13Mwitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa pamoja na kwamba matembezi hayo yalianza mapema saa moja na nusu mpaka saa mbili na robo.