Jumamosi, 27 Oktoba 2012

TANZIA; NSUBISI SAMUEL MWAKIPUNDA AMEFARIKI DUNIA.

TANZIA
FAMILIA YA  MAREHEMU MCHUNGAJI MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MZEE NSUBISI SAMUEL MWAKIPUNDA (MKURUGENZI WA ZAMANI WA IDARA YA MAELEZO)  KILICHOTOKEA SIKU YA JUMATANO TAREHE 24/10/2012.

MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU PUGU KINYEMWEZI DAR ES SALAAM.
HABARI ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.

KWA MAWASILIANO ZAIDI
+255655994499
“BWANA AMETOA BWANA, AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”
AMEN

Jumanne, 23 Oktoba 2012

SHEIKH FARID HADI AFIKISHWA MAHAKAMANI JANA.

Shekhe Farid wa Uamsho kizimbani

Written by Khatib Suleiman, Zanzibar
 
BAADA ya uvumi wa kutoweka na kusababisha ghasia visiwani hapa na kisha kuonekana, jana kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu(JUMIKI) maarufu kama Uamsho, Shekhe Farid Hadi Ahmed na wenzake saba walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za uchochezi na kusababisha fujo.
Hata hivyo, Mahakama ya Mwanakwerekwe ilikataa kutoa dhamana kwa viongozi hao hadi keshokutwa shauri lao litakaposikilizwa katika mahakama hiyo, kwa madai kwamba uchunguzi zaidi unahitajika katika matukio hayo.
Shekhe Farid na viongozi hao saba, walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mjini saa nne asubuhi katika msafara wa magari sita ya Polisi. Wengine waliofikishwa katika Mahakama ya Mwanakwerekwe ni kiongozi mwandamizi wa Uamsho, Shekhe Azan Khalid Hamdani (43), Mussa Juma Issa (37), Suleiman Juma (50), Hassan Bakari Suleiman (39), Mselem Ali Mselem (52) na Khamis S. Khamis.
Akisoma mashitaka yanayowakabili washitakiwa hao, Mwendesha Mashitaka wa Serikali Mohamed Ame, alidai washitakiwa hao walikwenda kinyume na kifungu 45(a) na (b) cha Sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar namba 6 ya mwaka 2004.
Akifafanua, Ame alidai Agosti 17 saa 11 jioni Magogoni mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, washitakiwa hao wakiongoza Jumuiya ya Uamsho walitoa matamko ya uchochezi yanayoashiria uvunjifu wa amani na kusababisha fujo na mtafaruku kwa Serikali katika sehemu ya mihadhara yao.
Wakili wa Washitakiwa, Abdalla Juma aliomba Hakimu kuwapa hati ya mashitaka na dhamana washitakiwa hao, kitendo ambacho kilipingwa na Wakili wa Serikali.
Awali Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ame Msaraka Pinja alisema baada ya kupitia hoja za kila upande, Mahakama iliona isikurupuke kutoa dhamana ili kulifanyia kazi zaidi shauri hilo.
“Mahakama imepitia maombi yote mawili kutoka kwa upande wa mashitaka na Wakili wa washitakiwa na kuona isikurupuke na ni bora kulifanyia uchunguzi zaidi shauri la dhamana,” alisema Msaraka. Kabla ya hapo, wafuasi wa Uamsho walijazana katika eneo la mahakama hiyo ambapo ulinzi uliimarishwa katika maeneo mbalimbali, ikiwamo jirani na jengo hilo.
Aidha, ulinzi uliimarishwa pia katika maeneo na barabara zinazokwenda na kuingia katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe kwa ajili ya kudhibiti fujo za wafuasi wa Uamsho. Hali ya usalama katika mji wa Unguja na maeneo mengine ya mitaa kwa sasa ni shwari huku vikosi vya SMZ vikifanya doria na kutawanya makundi mbalimbali ya vijana.
Kutoweka kwake Shekhe Farid alitoweka ghafla wiki iliyopita na kudaiwa na wafuasi wake kuwa alikuwa ametekwa na vyombo vya usalama jambo lililosababisha vurugu.
Katika vurugu hizo za Zanzibar, maskani mbili za CCM za Kisonge na Mwembeladu zilichomwa moto na pia baadhi ya wafuasi wa Uamsho kudaiwa kumwua Koplo Said Abdulrahman wa Polisi kwa kumkata mapanga.
Wakati hali ikiwa hivyo na kusababisha Polisi kuongeza ulinzi Zanzibar, Shekhe Farid aliibuka ghafla na kudai kuwa alikuwa ameshikiliwa na watu wasiojulikana ambao walikuwa wakimhoji kuhusu harakati za jumuiya hiyo lakini hawakumdhuru.
Hata hivyo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havikuwa vimemshikilia Shekhe Farid, alisema walilazimika kumkamata na viongozi wenzake ili kufahamu wapi alikuwa na kuthibitisha kama kweli alitekwa au la kabla ya kumfikisha mahakamani jana.

Ijumaa, 19 Oktoba 2012

SHEIKH PONDA NA WAFUASI WAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI, WANYIMWA DHAMANA HADI NOVEMBA MOSI.


 

 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (mwenye kanzu) akiwa chini ya ulinzi wa askari wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam baada ya kusomewa mashtaka ya wizi, uvunjifu wa amani na uchochezi.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akishuka katika gari lililomleta katika Mahakama ya Kisutu leo
 Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa (mwenye kanzu nyeupe mbele) akiwa katiika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alikofikishwa pamoja na wafuasi wanaomuunga mkono kama wanavyoonekana pichani. (Picha zote na Habari Mseto Blog).
 
 Hali ya ulinzi ilikuwa kama inavyoonekana, ambapo askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakilinda amani katika Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakitawanyika baada ya Sheikh Ponda na wafuasi wake kurejeshwa mahabusu. Chini; Sheikh Ponda akipanda gari kurejea mahabusu.

DAR ES SALAAM, Tanzania
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, na wafuasi wake 49 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijiji hapa leo mchana,
kwa kosa la uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya Shilingi milioni 59.


Sheikh Ponda wanaoshitakiwa pia uvamizi wa kiwanja namba 311/2/4 kilichoko Block T Chang’ombe ambacho ni mali ya Kampuni ya Agritanza,   wanatetewa na wakili wa kujitegemea Nassor Mansoor.

Wakati wakifikishwa na baadaye  kuondoka kwenye viwanja vya mahakama hiyo wakiwa ndani ya magari ya Polisi na Jeshi la Magereza, walikuwa wakisikika wakipaza sauti wakisema; ‘Allah Akbar, Allah Akbar’.
 
Sheikh Ponda pia amefikishwa mahakamani hapo akidaiwa kuwashawishi Waislamu kugomea zoezi la sensa ya watu na makazi, iliyofanyika mwezi uliopita nchini kote na kufanya zoezi hilo kufanyika kwa kusuasua.

Hali ya usalama kwenye mahakama ya Kisutu na maeneo ya jirani iliimarishwa mchana wa leo, wakati Sheikh Ponda aliyekamatwa jana na Jeshi la Polisi na kufikishwa Makao Makuu ya Jeshi hilo katikati ya jiji – akifikishwa hapo na Waislamu wengine walioshiriki uvamizi wa kiwanja Chang’ombe.

Baada ya kukamatwa juzi usiku na kufikishwa Kituo Kiuu cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam jana, baadhi ya Waislamu wanaomuunga mkono walivamia kituoni hapo kushinikiza kuachiwa kwa kiongozi wao, kabla ya polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Hali ya amani imekuwa tata nchini katika siku za karibu, tangu Ijumaa iliyopita, ambapo kundi la watu wanaosadikika kuwa ni Waislamu walivamia kituo cha polisi huko Mbagala Zakhiem wakishinikiza wakabidhiwe kijana aliyedaiwa kukojolea Msahafu.

Baada ya kushindwa kufanikisha azma hiyo, hasira zao zikaishia katika uvamizi wa makanisa, ambayo kadhaa yalichomwa moto, kuharibiwa na kuibiwa kwa vitu mbalimbali na polisi kuwakamata watu zaidi ya 120 kabla ya kuchujwa na kubaki 36 waliofikishwa mahakamani.

Hali haikuwa shwari pia Visiwani Zanzibar, ambako kikundi maarufu cha Uamsho kimefanya vurugu jana, wakimskaka kiongozi wao mkuu Sheikh Farid, aliyedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana juzi usiku.

Kesi ya Sheikh Ponda ambaye alinyimwa dhamana na wenzake itatajwa tena Novemba Mosi mwaka huu, ambapo watarudi mahakamani hapo.
Chanzo; Francis Dande

ASKARI POLISI AUAWA KIKATILI HUKO ZANZIBAR, KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WAANDISHI

 

Kamishna
wa Polisi Mussa Ali Mussa akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi
wa Habari akielezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa
Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo
umefanyika katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.

 PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR
Askari huyo Nd. Abdelhman alifikwa na umauti juzi usiku akiwa njiani akitokea kazini kwenda nyumbani majira ya saa 6.00 usiku ndipo alipovamiwa na kupigwa mapanga hadi kufa . Tukio hili linahusishwa na vurugu zilizofanywa na baadhi ya wafuasi wa UAMSHO tangu juzi mchana baada ya habari kuzagaa kuwa kiongozi wao Sheikh Hadi ametekwa.

Jumatatu, 15 Oktoba 2012

MTUHUMIWA WA USAFIRISHAJI MADAWA YA KULEVYA AACHIWA HURU, NI ALHAJI MINTANGA.


Alhaji Shaaban Mintanga akiwa chini ya ulinzi mkali wakati wa kesi yake.
Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Alhaji Shaaban Mintanga, leo ameachiwa huru baada ya kushinda kesi yake ya kukamtwa na madawa ya kulevya. Mintanga ameachiwa huru baada ya kusota rumande tangu April 4 mwaka 2008.

CAPE VERDE YAIHAIBISHA CAMEROON KWENYE KUWANIA KUFUZU MASHINDANO YA MATAIFA HURU YA AFRIKA.

Cameroon yabanduliwa nje

Wachezaji wa Cameroon
Wachezaji wa Cameroon
Cameroon leo imebanduliwa nje ya fainali za kuwania kombe la mataifa huru barani Afrika zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini, licha ya kushinda mechi yao ya raundi ya pili kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Cape Verde hii leo mjini Yaunde.
Cape Verde iliilaza Cameroon kwa mabao mawili kwa bila katika mechi yao ya raundi ya kwanza.
Kabla ya mechi hiyo Cameroon ilihitaji kuishina Cape Verde kwa zaidi ya magoli mawili ili kujikatia tikiti ya kushiriki katika fainali hizo.
Cape Verde ambayo imeorodheshwa nyuma ya Cameroon katika orodha ya timu bora ulimwenguni, imeandikisha historia kwa kufuzu kwa fainali hizo za kuwania kombe la mataifa huru barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuishinda Indomitable Lions kwa jumla la magoli matatu kwa mawili.
Katika mechi nyingine ya kufuzu, Ethiopia ilivaana na Sudan ambapo Ethiopia imeibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila.
Katika mechi ya raundi ya kwanza Sudan ilishinda kwa mabao matano kwa matatu.
Ethiopia sasa imefuzu kupitia sheria ya goli la ugenini baada ya timu hizo kufungana jumla ya magoli matano kwa matano.

Jumapili, 14 Oktoba 2012

SHINDANO LA UCHORAJI TOKA IMAGE PROFFESSION NA BASATA


Shindalo la Uchoraji Kwa Taasisi za Kielimu
Image Profession ikishirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa mara nyingine inatangaza kuanza kwa muhula mpya wa pili wa Shindano ya Uchoraji maalumu kwa Taasisi za elimu.
Shindano ambalo pia linajulikana Kama: Educational Drawing Competition au Image Profession Educational Drawing Competition, lina malengo ya kuibua vipaji katika fani ya uchoraji kwa kuzingatia uwekezaji kwa watoto na vijana.
Theme/Wazo kuu la mwaka huu: ART IMITATES LIFE au SANAA HUFUATISHA MAISHA
Makundi ya ushiriki

  • Chekechea,
  • Elimu ya Msingi,
  • Elimu ya Sekondari na  
  • Elimu  ya Juu
Kwa maelezo na taratibu za Shindano tembelea Facebook Page/Group “Tanzania Drawing Competition” au wasiliana na BASATA au
DRAWING COMPETITION – IMAGE PROFESSION,
P O BOX 92 DAR ES SALAAM.
SIMU: +255 222 664 740 / +255 713 484 040
/ +255 714 676 217 / +255 716 430 084

Jumamosi, 13 Oktoba 2012

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA SACP LIBERATUS BARLOW AMEUAWA USIKU WA KUAMKIA LEO.

BREAKING NEWS: RPC MWANZA AUAWA USIKU WA KUAMKIA LEO


 SACP Liberatus Barlow 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Barlow ameuawa usiku wa kuamkia leo katika tukio linalohusishwa na ujambazi. 

Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa baada ya kumrudisha dada yake kutoka katika kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili mnamo saa 7.30 usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mkuu wa operesheni wa jeshi la polisi ni kuwa habari hizo ni za kweli na amewataka wananchi wa mwanza kuwa watulivu na kuahidi wahalifu hao watapatikana.
Pole sana wanafamilia kwa kupoteza kiongozi mzuri wa jamii na familia.
Habari; ITV

Jumatano, 10 Oktoba 2012

AJALI ZINATUMALIZA, MWENDESHA BODABODA NA ABIRIA WAKE WAFA KWA AJALI MAENEO YA MAKONGO.


Jamaa akijaribu kutambua mwili wa marehemu juzi asubuhi waliofariki baada ya pikipiki yao kugongwa juzi asubuhi maeneo ya Makongo shuleni, Dar es salaam. Eneo hili limekuwa zikitokea ajali za mara kwa mara hasa pikipiki, tuchukue tahadhari.(Picha na Sufiani Mafoto)

Jumapili, 7 Oktoba 2012

MTU MZIMA RICK ROSS AMEPANDA JUKWAANI SAA 8.15 HADI 9.00 USIKU

Mtu mzima Rick Ross kutoka nchini Marekani hivi sasa yuko jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar salaam ,anakamua ile mbaya na mashabiki wamepagawa vyakutosha kwa kila anachowaelekeza kufuata wanafuata jamaa amefunika mbaya, hili ni onesho lake la kwanza nchini Tanzania kwa mwanamuziki huyo kufanya onesho Tanzania.
Mwanamuziki Rick Ross kabla ya kupanda jukwaani alitanguliwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa bongofleva hapa nyumbani ambapo nao walikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye viwanja vya Leaders

FIESTA 2012, RICK ROSS AMEWASILI TAYARI NA SHOO INAENDELEA HAPO LEADERS.

 Meneja wa Bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Allan Chonjo akisalimiana na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Rick Ross mara baada ya kuwasili usiku huu ndani ya uwanija wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,akiwa na baadhi ya wanamuziki wenzake pichani nyuma,kati ni Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd,Balozi Kindamba ambao ndio waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalotarajiwa kufanyika hapo kesho.Picha nyingine baadae kidoogo wadau.

Mashabiki waliohudhuria

Msanii Lina akitumbuiza katika utangulizi.
 

Alhamisi, 4 Oktoba 2012

MAMA MREMBO KIONGOZI WA MALAWI BADO ANG'ANG'ANIA ZIWA LOTE LA NYASA, ADAI RAMANI ZA TANZANIA ZIMEBADILISHWA, HATAKI MAZUNGUMZO.




President Joyce Banda told journalists in Lilongwe on Tuesday that the issue has gone too far and Malawi will seek international help to ensure that justice prevails, saying Malawians cannot entertain embarrassment whenever they want to fish on the lake.
“The lake issue has gone to next step. I have decided to take to International Court of Justice to determine and resolve this wrangle,” President Banda said.
Banda explained that government through Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation wrote their Tanzanian counterparts over the issue of producing new map that include part of Lake Malawi.
She said the agreed follow-up dialogue meeting that was supposed to be held in Tanzania was called off after realizing that they had produced new map, saying unless they have responded to the letter then Malawi can decide whether to go ahead with the meeting or not.
“We decided to call off the follow-up dialogue meeting over the lake issue after we discovered that Tanzania had issued a new map with part of our lake. If they don’t respond to our letter, we will look at alternatives.
“Government through Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation wrote them and we are waiting for their response,” she added.
President Banda returned home on Tuesday from United States of America where she attended the 67th United Nations General Assembly which started on September 25 through October 1, 2012.
During the Summit, President Banda made her first maiden speech at the General Assembly. In her speech, she commended the President of General Assembly on the theme as it offered an opportunity for world leaders to reflect on the devastating effects of conflicts on the lives of millions of people.
She also told the Assembly that achieving sustainable development for all was the best way to ensure a peaceful and stable world, saying the greatest threats to peace are poverty, lack of opportunity and hope.
The President also shared her vision of transforming Malawi by eradicating poverty through economic growth and wealth creation.

WATANI WA JADI WATOKA SARE YA 1-1

Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1

NewsImages/6620754.jpg
Nani mbabe leo?
Mtanange wa watani wa jadi, Simba na Yanga umeisha kwa kutopatikana mbabe kati ya timu hizo mbili za jijini Dar es Salaam. Mechi imeisha Simba 1 Yanga 1.
Simba walianza kwa kujipatia goli la kuongoza dakika ya nne tu kupitia kwa Amri Kiemba aliyeunganisha krosi ya Saidi Chollo.

Yanga walisawazisha kwa njia ya penalti dakika ya 65 kupitia kwa Saidi Bahanuzi.

Dakika ya 79, Simon Msuva wa Yanga alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Nyoso wa Simba.

Kikosi cha Simba kilichoanza leo:
Kaseja, Nassoro Masoud, Paul Ngalema, Shomari Kapombe, Juma Nyosso, Jonas Mkude, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Edward Christopher na Amri Kiemba. MFUMO 4-3-3


Kikosi cha Yanga kilichoanza leo:
Yaw Berko, Mbuyu Twite, Stephano Mwasika, Nadir Haroub, KelvinYondani, Athumani idd , Nizar Khalfan, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Said Bahanuzi