Jumapili, 16 Januari 2011

AJIRA KWA WALIMU

Serikali yatangaza ajira 9226 kwa walimu wa shule za sekondari na vyuo, Waziri wa Elimu Dr. Shukuru Kawambwa amesema walimu hao wanatakiwa kuripoti kwenye Halmashauri mbalimbali walizopangiwa ifikapo taerehe 24/01/2011. Malipo na stahili zao zote zitalipwa na Halmashauri husika. Orodha yao yapatikana kwenye tovuti zifuatavyo; (www.moe.go.tz) na (http://www.pmoralg.go.tz/)

KATIBA YA TANZANIA

KATIBA NI NINI?

Katiba ya nchi ni mkataba wa namna nchi itakavyoendeshwa ikizingatia masuala makuu ya msingi ikiwemo haki za raia,namna uongozi wa nchi utakavyopatikana, vipaumbele vya taifa mila na desturi za watu wa taifa husika. Mkataba huu ni kati ya wananchi na kikundi cha wananchi wachache walioteuliwa kuongoza wenzao.(viongozi)

Wananchi wanakubali kutoa madaraka ya kuongoza nchi yao kwa viongozi wao(serikali) ili watekeleze makubaliano yaliyomo ndani ya katiba kwa kufuata vigezo mbalimbali mfano serikari ikishindwa kuongoza vizuri basi itabidi iachie madaraka na wawekwe wengine watakaotekeleza mkataba ule.(katiba)

Hivyo basi watawaliwa wanajitoa na kukubali kukabidhi madaraka ya kuongozwa kwa kikundi kidogo cha watawala(dola) ambacho kina watu toka jamii ileile, ndio maana tunaita mkataba. Katiba ni sheria mama, mambo yote yatakayotekelezwa au sheria zitakazotungwa itabidi zifuate matakwa ya katiba ile, yasiwe kinyume. Mfano katiba ikisema; "Ardhi ni mali ya Rais wa Nchi, kila mwananchi ana haki ya kumiliki ardhi." Basi kusitokee itakayosema vinginevyo kama, Matajiri au mtu mmoja anaweza kumiliki ardhi kubwa na kuihodhi wakati wananchi wengine hawana hata kipande cha kulima bustani.

Jumatatu, 10 Januari 2011

HAPPY BIRTHDAY TO YOU

Happy birthday mkubwa
09/01 

 Maisha ni malengo na juhudi zinahitajika,usikate tamaa




 Mtu na dadaye
Mdau ameshaanza kuzeeka
Baba na mwana

Jumapili, 9 Januari 2011

HERI YA MWAKA MPYA 2011

 Abla from West Africa
 Nigerian students doing exams
 Kenyan girl
From Mswati's Kingdom.
All of them wishes you happy and prosperous new year 2011.

Alhamisi, 6 Januari 2011

MSIMU UMEISHA



Msimu wa mavuno na mauzo ya korosho umepita tayari,hata hivyo msimu haukuwa mzuri sana kwa eneo la kaskazini mwa Nachingwea ukilinganisha na kusini magharibi(Kilimarondo) ambako wao wamevuna sana.

SAFARI YA KUSINI MWA TZA.

Kijana wa kijiji cha Mandawa Nachingwea akitoka kisimani kuchota maji umbali wa kama km 3 hivi, wastani kila nyumba ina baiskeli moja kwa kazi hiyo.